Home » » YOUNG AREJEA MAN UNITED KUIVAA LIVERPOOL EUROPA LIGI

YOUNG AREJEA MAN UNITED KUIVAA LIVERPOOL EUROPA LIGI



Manchester United winger Ashley Young is all smiles as he returns to training ahead of his side's encounter with rivals Liverpool
 (Front to back) Anthony Martial, Memphis Depay and Ander Herrera take part in a running drill as they warm up ahead of the sessionRed Devils manager Louis van Gaal (centre) watches on as his group of players are put through their paces on Wednesday
WACHEZAJI wawili majeruhi wa Manchester United, Ashley Young na Cameron Borthwick-Jackson wako fiti kuelekea mchezo wa kesho wa Europa League dhidi ya mahasimu, Liverpool baada ya kupona maumivu yao. 
Young amerejea mazoezini baada ya miezi miwili ya kuwa nje na leo amefanya mazoezi wakati Manchester United ikijiandaa kwa mechi ya Europa League dhidi ya Liverpool Uwanjawa Old Trafford kesho usiku.
WInga huyo wa England hajaonekana uwanjani tangu United iifunge Liverpool 1-0 Uwanja wa Anfield Januari 17 baada ya kwenda kufanyiwa upasuaji Marekani kutokana na matatizo ya nyonga

Lakini haijajulikana kama Young atacheza kesho dhidi ya kikosi cha Jurgen Klopp baada ya kuwa nje kwa muda refu, lakini yuko vizuri. 
Nahodha Wayne Rooney, Phil Jones, Luke Shaw na Will Keane sasa wanabaki kuwa wachezaji pekee majeruhi, baada ya Cameron Borthwick-Jackson pia kufanya mazoezi leo asubuhi Uwanja wa Carrington.
Borthwick-Jackson hajacheza tangu United iifunge 3-0 Shrewsbury katika Kombe la FA February 22.
Kikosi cha Louis van Gaal kilionekana kipo vizuri kuelekea mchezo huo ambao wanahitaji kukipiku kipigo cha 2-0 walichopewa wiki iliyopita Uwanja wa Anfield kwa mabao ya Daniel Sturridge na Roberto Firmino ili kwenda Robo Fainali.
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger