Home »
» STARS YAWASILI SALAMA,KUKIPIGA NA CHAD JUMATATU YA PASAKA
STARS YAWASILI SALAMA,KUKIPIGA NA CHAD JUMATATU YA PASAKA
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KIKOSI
cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kimewasili Dar es
Salaam usiku huu wachezaji wake wakiwa wamechoka baada ya safari ndefu
tangu mchana kutoka D’jamena, Chad kupitia Addis Ababa, Ethiopia.
Mara
baada ya kuwasili, Taifa Stars walipokewa na Katibu wa Baraza la
Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja ambaye aliwapa hotuba fupi ya
mapokezi.
Stars
ambayo Jumatano iliwafunga wenyeji Chad 1-0 katika mchezo wa Kundi G
kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat
Ouya mjini D’jamena mara baada ya kuwasili, ilikwenda moja kwa moja
kambini, hoteli ya Urban Rose, katikati ya jiji.
|
Nahodha
Mbwana Samatta akiwaongoza wachezaji wake kutoka Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam baada ya kuwasili
usiku huu |
Wachezaji waliowasili na Taifa Stars usiku huu kutoka Chad ni makipa; Aishi Manula na Ally Mustafa ‘Barthez’.
Mabeki; Juma Abdul, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Kevin Yondan na David Mwantika.
Viungo; Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Himid Mao, Mohammed Ibrahim, Ibrahim Hajib, Deus Kaseke, Farid Mussa na Shiza Kichuya.
Washambuliaji ni John Bocco, Thomas Ulimwengu na Nahodha Mbwana Samatta.
|
Thomas Ulimwengu akitoka Uwanja wa Ndege baada ya kuwasili |
|
Katibu wa BMT, Mohammed Kiganja akiwahutubia wachezaji Uwanja wa Ndege |
|
Wachezaji wa Taifa Stars wakimsikiliza Katibu wa BMT |
|
Wachezaji wa Taifa Stars wakimsikiliza kwa makini Katibu wa BMT |
|
Baadhi ya viongozi na wachezaz wakitoka Uwanja wa Ndege baada ya kuwasli |
|
Kutoka
kulia ni Jonas Mkude, Aishi Mnula na Shiza Kichuya wakiwa Uwanja wa
Ndege wa Addis Ababa, Ethiopia wakisubiri kuunganisha ndege ya kuja Dar
es Saalaam |
Wachezaji
hao wataungana na wachezaji wengine sita waliobaki kambini Dar es
Salaam, ambao ni kipa Shaaban Kado, viungo Ismail Khamis ‘Suma’, Said
Ndemla na washambuliaji Elias Maguri, Jeremiah Juma na Abdillah Yussuf
‘Adi’.
Stars
inashika nafasi ya tatu katika Kundi G, ikiwa na pointi nne baada ya
kushinda mechi moja dhidi ya Chad, kufungwa na Misri 3-0 na kutoa sare
ya 0-0 na Nigeria.
Misri
inaongoza Kundi hilo kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Nigeria yenye
pointi nne sawa na Tanzania, lakini ina wastani mzuri wa mabao, wakati
Chad inashika mkia haina pointi.
0 comments:
Post a Comment