UCL, UEFA
CHAMPIONZ LIGI itakamilisha idadi ya Timu 8 kucheza Robo Fainali baada
ya Wiki iliyopita 4 kupatikana na Jumanne na Jumatano kutoa Timu
nyingine 4.Jumanne Usiku zipo Mechi mbili kati ya Atletico Madrid na PSV
Eindhoven huko Vicente Calderon Jijini Madrid baada ya Timu hizi kutoka
0-0 kwenye Mechi ya kwanza na nyingine ni ile itakayopigwa Etihad
Jijini Manchester huku Man City wakiwa kifua mbele baada ya kuinyuka
Dynamo Kiev 3-1 katika Mechi ya kwanza.(VICTOR)
TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA ROBO FAINALI:
-Real Madrid
-VfL Wolfsburg
-Paris St Germain
-Benfica
**Bado Timu 4
+++++++++++++++++++++
Mechi
nyingine 2 zitapigwa Jumatano Usiku na ile tamu kabisa ni ile ya Nou
Camp wakati Barcelona watarudiana na Arsenal huku wao wakiwa washindi wa
2-0 baada ya Mechi ya kwanza iliyochezwa Emirates.
Nyingine
ni huko Allianz Arena Jijini Munich huku Bayern Munich na Juventus
zikiwa zimetoka Sare ya 2-2 kutoka Mechi ya kwanza iliyochezwa Turin
Nchini Italy.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Marudiano
**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza
JUMANNE 15 MAR 2016
Atletico Madrid v PSV Eindhoven [0-0]
Man City v Dynamo Kiev [3-1]
JUMATANO 16 MAR 2016
Barcelona v Arsenal [2-0]
Bayern Munich v Juventus [2-2]
++++++++++++++++++++++++++++
TAREHE MUHIMU:
Raundi za Mtoano:
-Droo ya Robo Fainali: Machi 18
**Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13
-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15
**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4
FAINALI
Mei 28
San Siro, Milan, Italy
0 comments:
Post a Comment