Home » » MARCUS RASHFORD KUICHEZEA ENGLAND EURO 2016

MARCUS RASHFORD KUICHEZEA ENGLAND EURO 2016

ENGLAND-HODGSON

                                                                              MANUNITED-RASHFORD-PORTRAIT                                                                                                                                       MENEJA wa England Roy Hodgson ameacha mlango wazi kwa Chipukizi wa Manchester United Marcus Rashford kuwemo kwenye Kikosi chake kitakachocheza Fainali za Mataifa ya Ulaya, EURO 2016, huko France Mwezi Juni.

Rashford, Kijana wa Miaka 18 mzaliwa wa Jiji la Manchester, aliibuka ghafla kwenye Kikosi cha Kwanza cha Man United Wiki iliyopita na kupiga Bao 2 walipoitwanga FC Midtjylland 5-1 na kufuzu kuingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI na kisha Mechi inayofuatia kupiga tena Bao 2 wakati Man United inaibomoa Arsenal 3-2.  
Rashford ametinga Kikosi cha Kwanza cha Man United baada ya kuumia kwa Wayne Rooney na Anthony Martial lakini kwa umahiri na kipaji alichoonyesha sasa ni wazi atabaki Kikosini hadi mwishoni mwa Msimu.
Kijana huyo ameshawahi kuichezea Timu ya Taifa ya Vijana ya England ya chini ya Miaka 18, U-18.
++++++++++++++++++++++++
EURO 2016
MAKUNDI:
KUNDI A: France, Romania, Albania, Switzerland.
KUNDI B: England, Russia, Wales, Slovakia.
KUNDI C: Germany, Ukraine, Poland, Northern Ireland.
KUNDI D: Spain, Turkey, Czech Republic, Croatia.
KUNDI E: Belgium, Republic of Ireland, Sweden, Italy.
KUNDI F: Portugal, Iceland, Austria, Hungary.
Fainali zitafanyika lini:
-Euro 2016 itaanza Ijumaa Juni 10 na kumalizika Jumapili Julai 10.
-Hii ni mara ya kwanza kwa Fainali hizi kuwa na Timu 24 na hivyo itakuwepo Raundi ya Mtoano ya Timu 16, kisha Robo Fainali na Nusu Fainali.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Na Kocha Roy Hodgson, akiongea akiwa kwenye Warsha ya Makocha wa Timu za EURO 2016 huko Paris, France, amepinga kwamba hamna uwezekano wa Rashford kuwemo kwenye Kikosi chake.
Hodgson amesema: “Siwezi kusema yumo au hayumo, nategemea tu afanye vizuri.”
Aliongeza: “Nimekuwa nikimtazama Rashford kwa Miaka Miwili. Yupo kwenye Timu zetu. Anachezea England U-18, hivyo tunafurahi Mchezaji wetu tunaemwamini na ambae ana hatima nzuri anapata nafasi kuchezea Timu ya Kwanza!”
“Hilo ni jambo jema na naomba liendelee hadi mwishoni mwa Msimu. Kufunga Bao 4 kwa Mechi 3 ni kitu kikubwa mno na kama ataendeleza hilo ni jambo jema kwa Manchester United na England!”
Maneno ya Hodgson yametia imani kubwa kwamba Kijana huyo ana nafasi kubwa kwenda EURO 2016 hasa kutokana na desturi ya Kocha huyo wa England kuchukua Vijana wabichi kwenye Mashindano makubwa.
Hodgson amefafanua: “Nadhani tushatoa nafasi kwa Vijana na Klabu pia zinabahatisha kwa kutumia Vijana. Alex Oxlade-Chamberlain alikuwemo 2012, Sterling alikuwemo Kikosini akiwa na Miaka 18, 19. Wapo wengi tu, yupo pia Ross Barkley.”
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger