Johan
Cruyff (kulia) akiwa na Mtendaji Mkuu wa BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE,
Mahmoud Zubeiry enzi za uhai wake alipozuru Tanzania mwaka jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA
GWIJI wa soka, Mholanzi Johan Cruyff amefariki dunia akiwa ana umri wa miaka 68.
Cruyff,
ambaye aliichezea mechi 48 Uholanzi pamoja na klabu za Ajax ya kwao na
Barcelona ya Hispania, amefariki dunia leo baada ya kusumbuliwa na
ugonjwa wa saratani.
Taarifa
katika tovuti yake imesema; "Machi 24 mwaka 2016 Johan Cruyff (miaka
68) amefariki dunia kwa amani mjini Barcelona, akiwa amezungukwa na
famili yake baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa saratani,".
"Ilikuwa ni huzuni kubwa na tunakuomba uheshimu siri za familia katika wakati huu mgumu,".
Cruyff,ambaye
ameshinda mataji matatu ya Ulaya na manane ya Uholanzi akiwa na Ajax,
ameanza kusumbuliwa na saratani tangu Oktoba mwaka jana.
Aprili mwaka jana, Cruyff
alizuru Tanzania pamoja na kikosi cha Maveterani wa Barcelona ambao
walicheza mechi ya wachezaji wa zamani nchini Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
0 comments:
Post a Comment