Gari ya kwanza ya Benzi
Historia ya motokaa
Kwa karne nyingi watu walitumia magari yaliyovutwa na
wanyama kwa mfano farasi,
punda au maksai. Waroma wa kale walifanya
majaribio na magari yaliyosukumwa na watumwa. Maendeleo ya uhandisi
yalisababisha majaribio ya kutengeneza magari yaliyosogezwa kwa nguvu ya upepo
yakitumia tanga
kuanzia mwaka 1600 huko Uholanzi.
Injini za mvuke
Baada ya kugunduliwa kwa injini
ya mvuke nguvu yake ilitumiwa pia kwa vyombo vya usafiri. Kutokana na uzito wa injini pamoja
na magari yaliyoweza kuvumilia uzito mkubwa wa injini pamoja na maji na kuni
iliyohitajika kuchemsha maji vyombo hivi havikufaa barabara za kawaida
vikatumia njia ya reli
za chuma. Nusu ya pili ya karne ya 19 iliona maendeleao ya kutengenezwa kwa
motokaa za mvuke madogo yaliyotembea barabara za kawaida katika nchi za Ulaya
na Marekani.
Gari ya Ford
Injini za umeme
Sehemu ya pili ya karne ya 19 iliona pia magari
yaliyoendeshwa kwa nguvu ya umeme. Magari haya yana faida nyingi; muundo wa
gari ni rahisi zaidi kwa sababu haihitaji giaboksi wala gia na gari halina makelele
pia hautoi herufu baya ya eksozi. Lakini magari haya yalikuwa na
tatizo ya kwamba yalitegemea kupata nichati kwa njia ya beteri nzito zilizochukua muda mrefu
kuchajiwa. Hata hivyo hadi mwanzo wa karne ya 20 magari ya umeme yalikuwa mengi
katika miji mikubwa.
Basi ya umeme mjini San
Francisco inapokea nishati kupitia waya juu ya barabara inapopita
Mwaka 1900 asilimia 40 za motokaa zote nchini Marekani
zilikuwa na injini za mvuke, 38 % za umeme na 22% za petroli. Mjini New York nusu
ya motokaa zote zilikuwa na injini ya umeme.
Baadaye magari ya petroli yalisogea mbele kwa sababu
yaliweza kutembea mbali kwa kujaza mafuta kuliko gari la umeme kwa beteri yake
tena beteri ilichua masaa hadi kujazwa upya wakati mafuta hujazwa mara moja.
Katika nchi kadhaa mabasi ya umeme yameendelea kutumiwa katika
miji mikubwa yakipokes nishati si kwa beteri bali kwa nyaya za umeme
zinazopangwa juu ya barabara ambako basi inapita.
Injini za mwako ndani (petroli na diseli)
Injini mwako ndani imekuwa
hadi leo njia kuu ya kusogeza magari na kwa kawaida tukiongelea motokaa
tunamaanisha gari lenye injini mwako ndani inayochoma petroli au diseli.
Motokaa ya kwanza ya Benz ya 1885
Katika karne ya 19 wahandisi
mbalimbali walianza
kutengeneza injini za mwako wa ndani zilizochoma gesi au petroli ndani
yake.
Injini ya kwanza iliyofaulu kuanzia 1876 na kutengenezwa kwa wingi
ilikuwa ni ile ya Mjerumani Nikolaus Otto aliyeshirikiana na Gottlieb
Daimler na Wilhelm Maybach. Ilikuwa na mapigo manne petroli ikichomwa
kwa msaada wa mwasho wa
umeme na hadi leo sehemu kubwa ya injini zote inafuata kielelezo wa Otto. 1879 Karl Benz alitengeneza injini ya
mapigo mawili kwa mfano wa Otto akaitumia kwa gari lake na tangu 1885 akatoa
aina ya kwanza ya motokaa yenye magurudumu matatu iliyoendelea kujengwa
mfululizo yaani kibiashara.
Maendeleo ya motokaa zilizotumia injini mwako ndani
yalikuwa haraka. Mwanzoni yalikuwa na matatizo mengi hasa uhaba wa petroli.
Benz alinunua mafuta kwa gari lake kwenye duka la dawa.
1892 mhandisi Mjerumani Rudolf Diesel alitunga injini
inayochoma mafuta kwa kuikandamiza vikali na kutumia joto la hewa ndani ya
injini kutokana na mshtuko wa kukandamizwa. Mashine hizi zina uwezo kutumia
aina mbalimbali za mafuta na ile ya kawaida ilikuwa nzito kuliko petroli
ikaitwa "diseli". Injini za diseli zamani hazikupendwa kwa magari
madogo kutokana na sauti kubwa zaidi ya injini lakini zikawa kawaida kwa malori, mabasi na injini
za meli kwa sababu zinatumia mafuta kidogo kuliko injini za petroli.
Ushindi wa motokaa
Mwanzoni motokaa zilikuwa ghali sana zikanunuliwa na
matajiri pekee. Mwaka 1914 mhandisi wa Marikani Henry Ford
alianza kutengeneza gari lake la "Ford Model T" kiwandani akitumia
mbinu mpya; aligawa matengenezo ya gari kwa hatua mbalimbali zilizotekelezwa na
wafanyakazi walioshughulika hatua moja-moja tu. Mbinu huu ulisababisha
utekelezaji wa haraka kwa sababu kila mfanyakazi alikuwa na shughuli chache zu
alizojua kwa undani kabisa akiwa na vifaa na vipuri vyote pale alipofanya kazi
bila kupotezy muda. Kwa njia hii Ford aliweza kutengeneza magari mengi tena kwa
bei nafuu na hata watu wenye mapato ya wastani waliweza kununua gari hili.
Mfanyakazi wa Ford aliweza kununua gari kwa mshahara wa miezi minne. Kwa jumla
magari milioni 15 ya Ford T yalitengenezwa hadi 1927.
Wengine waliiga mfano wa Ford na motokaa zilizidi
kupanua. Baada ya vita kuu ya pili ya dunia polepole katika
nchi nyingi za Ulaya, Amerika na Asia motokaa ilikuwa njia ya kawaida ya
usafiri kwa watu wengi.
Upanuzi wa usafiri wa motokaa ulibadilisha tabia
nyingi za nchi zilizoathiriwa nao. Miji ilibadilika kwa kutengeneza barabara
pana za kupokea magari mengi. Watu walianza kuishi mbali na mahali pa kazi kwa
sababu usafiri ulikuwa rahisi na haraka. Njaa ya petroli na diseli iliendelea
kuzidi na nchi zenye akiba za mafuta
ya petroli zilitajirika kwa mfano nchi za Uarabuni, Norwei au Venezuela.
0 comments:
Post a Comment