Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini (TFF) jana limefanya Mkutano Mkuu wa Mwaka
katika Ukumbi wa hoteli ya Regal Naivera jijini Tanga ambapo mgeni Rasmi
alikua ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza.
Katika hotuba yake kwa wajumbe wa mkutano huo, Mahiza aliushukuru
uongozi wa TFF nchini kwa kuweza kuandaa mkutano mkuu mzuri na wa kisasa
ambao pia ulifanyikia katika mkoa wake wa Tanga.
Akiongea na wajumbe wa mkutano mkuu, Mahiza alisema, TFF ina
changamoto ambazo inapaswa kuzifanyia kazi kwa na hasa katika kuendeleza
soka la wanawake nchini ambalo bado mwamko wake uko chini sana.
Mahiza alisema, Mpira wa miguu kwa sasa ni ajira nzuri ambayo
inasaidia kujikwamua kiuchumi kwa wachezaji pamoja na familia zao,
nayaomba makamouni yajitokeze kuwekeza katika mpira wa miguu na hasa
katika soka la wanawake.
“Mahitaji ya wanawake katika kushiriki/kucheza mpira wa miguu ni
makubwa zaidi, tofauti na wanaume hivyo kuangalia jinsi gani wadhamini
wanapatikana ili kuweza kuwasaidia wanawake” alisema Mahiza.
Mkutano ulijadili Ajenda za kawaida ambazo ni Kufungua Mkutano ni
Uhakiki wa Wajumbe, Kuthibitisha Muhtsari wa Mkutano Mkuu uliopita,
Yatokanayo na Mkutano uliopita, Hotuba ya Rais, Taarifa kutoka kwa
Wanachama, Kuthibitisha ripoti ya utekelezaji wa Kamati ya Utendaji.
Zingine ni Kuthibitisha ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu 2013,
Kuthibitisha ripoti ya Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu, Kupitisha bajeti ya
2015, Marekebisho ya Katiba, Mengineyo na Kufunga Mkutano.
Baada ya majadiliano ya kina mkutano mkuu pia uliazimia kuahirisha
ajenda ya marekebisho ya Katiba hadi Mkutano Mkuu ujao utakaofanyika
mwezi Disemba mwaka huuu.
Wakati
huo huo Leo Jumapili asubuhi Mkuu wa Mkoa Tanga, Mwantumu Mahiza
ameweka jiwe la msingi katika eneo la kituo cha michezo cha kukuzia
vipaji lilipo eneo la Mikanjuni jijini Tanga.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa uwekaji jiwe la msingi, Mahiza
alisema wamejisikia faraja mkoa wa Tanga kupata nafasi hiyo kuwa mkoa wa
kwanza kupata kituo cha kukuzia vipaji nchini.
Mahiza alisema uongozi wa Serikali mkoa wa Tanga utashirikiana na
Chama cha Mpira wa Miguu mkoa wa Tanga (TRFA)/TFF katika kusaidia
usimamizi wa uendeshaji wa kituo hicho.
Mahiza ameishukuru TFF kwa kuamua kuwekeza katika ujezi wa kituo
hicho, ambacho baaade kitatoa nafasi kwa vijana kupata ajira kupitia
mpira na shughuli nyingin
0 comments:
Post a Comment