Home » » Ndalichako ‘akomaa’ na maofisa elimu

Ndalichako ‘akomaa’ na maofisa elimu

Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
HOFU ya utumbuaji majipu kwa sasa imetanda kwa Maofisa Elimu Msingi na Sekondari ambao wamekuwa wakidaiwa kufanya ufisadi wa kutumia fedha za umma kwa manufaa yao, anaandika Dany Tibason.
Hofu hiyo imetokana na Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Mafunzo ya Ufundi na Teknolojia kutangaza kiama kwa maofisa wanaotumia fedha hizo kinyume na makusudio.
Prof. Ndalichako akifunga mkutano wa tatu wa Maofisa Elimu Mkoa na Wilaya kwa Shule za Msingi na Sekondari (REDEOA) amesema kwamba, amegundua kuwepo kwa ufisadi katika fedha Sh 66 Bilioni zilizotengwa kwa ajili ya mfunzo, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule nchini.
Amesema baadhi ya fedha hizo zilitolewa bila kufuata utaratibu sahihi na hivyo kufanya wengine kutofahamu kama kuna fedha kama hizo zimetolewa.
Katika hotuba yake Prof. Ndalichako bila kumtaja ofisa elimu kuna mtu alitumia Sh 60milioni kukarabati darasa moja la Shule ya Msingi.
“Hiyo ni ukarabati wa darasa tu la Shule za Msingi. Wale waliokula fedha hizo nawaambia zitawatokea puani, hatuwezi kuwavumilia watu ambao ni mafisadi wasiokuwa na huruma ,”amesema.
Katika hatua nyingine Prof . Ndalichako amesema amezuia mafunzo yalikuwa ya gharimu Sh 4 bilioni ambapo mtu mmoja alitengewa Sh milioni 4 kwa ajili ya semina ya siku nne.
“Inamaana kila mtu alikuwa alipwe shilingi milioni moja kwa siku. Kweli hatuoni aibu kutumia fedha hizo kwa mafunzo. Watu wale wale wanaoenda kwa mafunzo yale yale hakuna impact (matokeo),”amesema.
Hata hivyo amesema wakati hayo yote yakitendeka wanafunzi wananyeshewa mvua kwa kukosa madarasa wanakaa chini kwa kukosa madawati.
Pia amesema, amemuita mmoja wa watu walioandaa mafunzo yenye kugharimu Sh 20 bilioni ili amfafanulie matumizi ya fedha hizo.
Akimkaribisha mgeni rasmi, Mwenyekiti wa REDEOA, Juma Kaponda ameshauri walimu wa Shule za Msingi waimarishwe kwa maarifa na lugha ya kingereza.
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger