Home »
» Manchester United wamepokea kichapo Anfield dhidi ya Liverpool
Manchester United wamepokea kichapo Anfield dhidi ya Liverpool
Usiku wa March 10 michuano ya Europa League iliendelea kwa michezo kadhaa kupigwa Barani Ulaya, Uingereza kulikuwa kuna mchezo wa kuvutia zaidi baina ya Liverpool dhidi ya Manchester United katika dimba la Anfield.
Roberto Firmino akishangilia goli
Takwimu za vilabu hivi kabla ya mchezo huu kupigwa , Man United alikuwa na takwimu nzuri licha ya kupokea kipigo cha goli 2-0 kwa mujibu wa mechiza mwisho za Manchester United na Livepool walivyokutana, Man Unitedalikuwa kashinda mara nne na Liverpoolmara moja
Hata hivyo takwimu hizo hazikuwa na msaada wowote kwa Man United kwani vijana wa Jurgen Klopp walifanikiwa kuifunga Man United kuanzia dakika ya 20 kupitia kwa Danny Sturridge kwa mkwaju wa penati, kabla ya dakika ya 73′ Roberto Firmino kupachika goli la pili lililoimaliza Man United na kufanya mchezo umalizike kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
unaweza kuyatazama hapa magoli ya Liverpool vs Manchester United
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari
0 comments:
Post a Comment