>>JUMAPILI SIMBA V MBEYA CITY, TAIFA!
LIGI KUU VODACOM, VPL, Jumamosi inaingia kwenye hatua muhimu sana kwa Mechi kali sana ya Vinara Yanga na Azam FC kupambana Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Yanga
na Azam FC, zote zikiwa zimecheza Mechi 19, zina Pointi 46 kila mmoja
lakini Yanga yupo Namba Moja kwa Ubora wa Magoli kwa Kufunga Goli 44,
Kufungwa 9, Tofauti ya Mabao ni 35 wakati Azam FC Kufunga 34, Kufungwa
11 Tofauti 23.
Kwenye Mechi ya kwanza ya VPL Msimu huu, Yanga na Azam FC zilitoka Sare ya Bao 1-1 hapo Oktoba 17.
Akizungumzia
kuhusu Mechi yao hii, Kocha wa Yanga kutoka Uholanzi, Hans van der
Pluijm, ambae Kikosi chake kimejichimbia Kambini huko Visiwani Pemba,
amesema Mechi ni ngumu lakini wao wamejitayarisha kwa ushindi tu.
Pluijm
alieleza: “Ni mchezo mgumu kwa Timu zote mbili, lakini hatuna budi
kupambana kupata ushindi utakaotupatia nguvu kuelekea kutetea ubingwa
wetu, lakini pia kuwafuata APR, tukiwa na matumaini ya ushindi kutokana
na kikosi kuwa na ari ya kufanya vizuri,”
Mara
baada ya Mechi hii na Azam FC, Jumatano ijayo Yanga watapaa kwenda
Kigali, Rwanda kupambana na APR ya Rwanda katika Mechi ya Kwanza ya
Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONS LIGI.
Nayo
Timu inayoshika Nafasi ya 3 kwenye VPL, Simba, ambao wamecheza Mechi 20
na wana Pointi 45, Jumapili wapo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam
kuivaa Mbeya City ambayo ipo Nafasi ya 10 ikiwa na Pointi 21 kwa Mechi
20.
Home »
» RATIBA YA LIGI KUU TANZANIA BARA (VPL) KWA WIKIENDI HII HIPO HAPA
0 comments:
Post a Comment