Home »
» MATOKEO YA EMIRATES FA CUP NCHINI ENGLAND
MATOKEO YA EMIRATES FA CUP NCHINI ENGLAND
Man United na West Ham zitapaswa kurudiana huko Upton Park ili kupata Mshindi wa kutinga Nusu Fainali ya EMIRATES FA CUP baada ya kutoka Sare ya 1-1 huko Old Trafford.
Hadi Mapumziko Mechi hii ilikuwa 0-0 na Kipindi cha Pili Dakika ya 68 West Ham walitangulia kufunga kwa Frikiki ya Dimitri Payet na Anthony Martial kusawazisha Dakika ya 83.
Mapema Leo, Mabingwa Watetezi Arsenali, wakiwa kwao Emirates walifungwa 2-1 kwa Bao za Odion Ighalo na Adlene Guedioura za Dakika za 50 na 63 na Arsenal kupata kifutia machozi toka kwa Danny Welbeck Dakika ya 88 ambae pia alikosa Bao la wazi la kusawazisha Dakika za Majeruhi.
Watford sasa wameungana na Crystal Palace na Everton kwenye Nusu Fainali.
Droo ya kupanga Mechi za Robo Fainali itafanyika Jumatatu Usiku Machi 14.
THE EMIRATES FA CUP 2015/16
Raundi ya 6-Robo Fainali
Ijumaa Machi 11
Reading 0 Crystal Palace 2
Jumamosi Machi 12
Everton 2 Chelsea 0
Jumapili Machi 12
Arsenal 1 Watford 2
Man United 1 West Ham 1
TAREHE MUHIMU
Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali
Jumamosi 21 Mei 2016
0 comments:
Post a Comment