Home » » MBEYA CITY KUWAKOSA WATATU DHIDI YA STEND UNITED

MBEYA CITY KUWAKOSA WATATU DHIDI YA STEND UNITED


 
 
MBEYA City iliyo katika harakati za kujinusuru kushuka daraja, itamkosa kiungo wake 'Mtu mzima Dawa', Haruna Moshi 'Boban' (pichani kushoto) katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Stand United kesho Uwanja wa Sokoine mjini hapa.
Boban atalazimika kusubiri mpaka Machi 14 kuingia tena kwenye kikosi cha City kufuatia kusumbuliwa na ugonjwa wa Maralia.
Mkuu wa kitengo cha utabibu Mbeya City, Dk Joshua Kaseko ameiambia  UKURASA WA HABARI kwamba Boban alianza kusumbuliwa na Malaria baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba Jumapili.
“Ni wazi hatakuwa sehemua ya mchezo kesho, ana Maralia tumekwishamtaarifu mwalimu (Kinnah Phiri) juu ya hili na tayari ameanza kufanya mazoezi maalumu na yule atakayechukua nafasi yake, imani yangu kubwa kuwa atakuwa sehemu ya kikosi march 14 wakati tutakapokuwa tunacheza na Africans Sports jijini Tanga" alisema Dk. Kaseko.
Kaseko amesema pia kiungo mwingine wa kati, Kenny Ally Mwambungu ataukosa mchezo wa kesho kutokana na kuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za jano mfululizo, wakati beki Deo Julius ataendelea kuwa nje kwa maumivu ya goti.

Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger