Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anazidi
kuendelea kuisuka Serikali yake ili iwe yenye ufanisi zaidi. Leo March
19 amefanya uteuzi ambao umeziba baadhi ya nafasi zilizokuwa wazi. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo.
Rais Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara
kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF). Prof.
Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ramadhan Dau, ambaye
ameteuliwa kuwa Balozi.
Aidha Rais Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha
kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Dkt.
Rioba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye
amestaafu.
Rais Magufuli amemteua pia Dkt. Mussa Iddi Mgwatu
kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania
(RAHCO). Dkt. Mgwatu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi
Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
0 comments:
Post a Comment