Home » » PHIRI: JOTO KALI LIMESABABISHA TUPIGWE 2-0 NA SPORTS

PHIRI: JOTO KALI LIMESABABISHA TUPIGWE 2-0 NA SPORTS




KOCHA Mkuu wa Mbeya City, Kinnah Phiri amesema kwmaba hali ya hewa nzito ilichangia kufungwa mabao 2-0 na wenyeji African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
“Hatukuwa na hali nzuri kimchezo, hali nzito ya hewa imetuathiri sana, tumecheza kukiwa na kiwango kikubwa cha joto, hata hivyo ndivyo matokeo ya soka yalivyo  tulichokitarajia  hakikuwa, tunakwenda Songea kwa mchezo mwingine, imani yangu  tunaweza kupata ushindi huko” alisema.
Katika mchezo wa jana, dakika 45 za kipindi cha  kwanza zilimalizika kwa timu hizo zikiwa hazijafungana,licha ya kuwepo kwa mashambulizi kadhaa pande zote mbili ikiwemo lile la  dakika ya 15 lililofanywa na Abdalah Juma  wa City  aliyefanikiwa kuwatoka mabeki wa Sports, lakini shuti lake  likashindwa kulenga lango.
Kipindi cha pili kilikuwa  kizuri kwa Sports  kwani walipanga mashambulizi vizuri na kufanikiwa kulifikia lango la City mara kadhaa ikiwemo dakika  60  ambapo  Omary Ibrahim alifanikiwa kuiandikia timu yake bao la kuongoza kwa mpira mzuri wa adhabu kufuati yeye mwenyewe kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari la City.
Mpira ukiwa unaelekea  ukingoni Ibrahim tena  alifanikiwa kufunga bao la pili kwa  Sports  baada ya kuuwahi mpira aliotanguliziwa na Salum Isihaka na kufanikiwa kuwatoka walinzi wa City kisha  kufunga  akiwa pembeni kidogo mwa lango.
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger