13:45 | Aston Villa | v | Chelsea | Villa Park | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
16:00 | Arsenal | v | Watford | Emirates Stadium | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
16:00 | Bournemouth | v | Manchester City | Vitality Stadium | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
16:00 | Norwich City | v | Newcastle United | Carrow Road | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
16:00 | Stoke City | v | Swansea City | Britannia Stadium | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
16:00 | Sunderland | v | West Bromwich Albion | Stadium of Light | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
16:00 | West Ham United | v | Crystal Palace | Boleyn Ground | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND KWA WIKIENDI HII HIPO HAPA
Messi Atua manchester City,ajifunga miaka 5
Mshambuliaji wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Leo Messi amejiunga na timu ya manchester city kwa ada ya paund million 200.Messi amesaini mkataba wa miaka 5 katika klabu hiyo inayomilikiwa na waharabu.
Messi amekua mchezaji ghari kununuliwa duniani baada ya kununuliwa kwa pesa nyingi na kumfunika mpinzani wake wa karibu Cristiano Ronaldo ambaye mwaka 2009 alinunuliwaa kwa paundi milllion 80 akitoka Man u kwenda Real madridi
(wajinga ndiyo waliwao, tusherehekee siku ya wajinga duniani, April Fouls!!)
CHAD WAJITOA AFCON
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
TIMU ya taifa ya Chad imejitoa kwenye mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani na maana yake mchezo kati yao na Tanzania uliokuwa ufanyike kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hautakuwepo.
Katika barua yao kwenda Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Chad wamesema wamejitoa kwa sababu za kiuchumi kwamba hawana fedha za kuwawezesha kuendelea na mechi za Kundi G.
Chad
inajitoa baada ya kukamilisha mechi tatu za mzunguko wa kwanza,
ikifungwa zote 2-0 na Nigeria ugenini, 5-1 na Misri nyumbani na 1-0 na
Tanzania nyumbani Jumatano.
Sasa Kundi G linabaki na timu tatu ambazo ni Tanzania, Nigeria na Misri.
Chad hawajaja Tanzania na maana yake mechi ya kesho na Taifa Stars haitakuwepo, lakini bado CAF haijatoa taarifa yoyote juu ya hilo.
Wenyeji Tanzania wamekuwa kambini hoteli ya Urban Rose, katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwa maandalizi tangu warejee kutoka D’jamena, Chad Alfajiri ya Ijumaa baada ya mchezo wa kwanza walioshinda 1-0 Jumatano iliyopita.
Inaonekana kipigo cha Taifa Stars nyumbani kilichotokana na bao pekee la Mbwana Samata dakika ya 30 akimalizia krosi ya Farid Mussa ndicho kimewafanya Chad wajitoe wakiamini hawana nafasi tena na hapa sababu za kiuchumi zinakuwa kisingizio tu.
Kujitoa kwa Chad ni hasara kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilioingia gharama za maandalizi ya mchezo wa marudiano, ikiwemo kuandaa tiketi za mchezo.
Kama Chad wangekuwa na majibu ya mapema japo baada ya mchezo wa kwanza tu D’jamena, TFF isingeingia gharama za ziada na ingevunja kambi, au ingeandaa mchezo wa kirafiki.
Aidha, kujitoa kwa Chad kumewanyima nafasi Watanzania kumuona kwa mara ya kwanza mshambuliaji Abdillah Yussuf ‘Adi’ wa timu ya Daraja la Pili England, Mansfield Town aliyejiunga na kambi ya Taifa Stars kwa mara ya kwanza safari hii.
Ndoto za mshambuliaji wa Mansfield Town ya Daraja la Pili England, Abdillah Yussuf ‘Adi’ kuichezea Taifa Stars kwa mara ya kwanza zimeyeyuka
Wachezaji waliokuwa kambini Taifa Stars chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco kwa maandalizi ya mchezo huo ni makipa; Shaaban Kado, Aishi Manula na Ally Mustafa ‘Barthez’.
Mabeki; Juma Abdul, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Kevin Yondan na David Mwantika.
Viungo; Ismail Khamis ‘Suma’, Said Ndemla, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Himid Mao, Mohammed Ibrahim, Ibrahim Hajib, Deus Kaseke, Farid Mussa na Shiza Kichuya.
Washambuliaji ni John Bocco, Thomas Ulimwengu, Nahodha Mbwana Samatta, Elias Maguri, Jeremiah Juma na Yussuf Adi.
Stars inashika nafasi ya tatu katika Kundi G, ikiwa na pointi nne baada ya kushinda mechi moja dhidi ya Chad, kufungwa na Misri 3-0 na kutoa sare ya 0-0 na Nigeria.
Misri inaongoza Kundi hilo kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na Nigeria yenye pointi tano. Misri na Nigeria wanarudiana Jumanne Cairo baada ya kutoa sare ya 1-1 Jumapili Kaduna.
TIMU ya taifa ya Chad imejitoa kwenye mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani na maana yake mchezo kati yao na Tanzania uliokuwa ufanyike kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam hautakuwepo.
Katika barua yao kwenda Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Chad wamesema wamejitoa kwa sababu za kiuchumi kwamba hawana fedha za kuwawezesha kuendelea na mechi za Kundi G.
Barua ya Chad kujitoa kufuzu AFCON |
Sasa Kundi G linabaki na timu tatu ambazo ni Tanzania, Nigeria na Misri.
Chad hawajaja Tanzania na maana yake mechi ya kesho na Taifa Stars haitakuwepo, lakini bado CAF haijatoa taarifa yoyote juu ya hilo.
Wenyeji Tanzania wamekuwa kambini hoteli ya Urban Rose, katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwa maandalizi tangu warejee kutoka D’jamena, Chad Alfajiri ya Ijumaa baada ya mchezo wa kwanza walioshinda 1-0 Jumatano iliyopita.
Inaonekana kipigo cha Taifa Stars nyumbani kilichotokana na bao pekee la Mbwana Samata dakika ya 30 akimalizia krosi ya Farid Mussa ndicho kimewafanya Chad wajitoe wakiamini hawana nafasi tena na hapa sababu za kiuchumi zinakuwa kisingizio tu.
Kujitoa kwa Chad ni hasara kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilioingia gharama za maandalizi ya mchezo wa marudiano, ikiwemo kuandaa tiketi za mchezo.
Kama Chad wangekuwa na majibu ya mapema japo baada ya mchezo wa kwanza tu D’jamena, TFF isingeingia gharama za ziada na ingevunja kambi, au ingeandaa mchezo wa kirafiki.
Aidha, kujitoa kwa Chad kumewanyima nafasi Watanzania kumuona kwa mara ya kwanza mshambuliaji Abdillah Yussuf ‘Adi’ wa timu ya Daraja la Pili England, Mansfield Town aliyejiunga na kambi ya Taifa Stars kwa mara ya kwanza safari hii.
Ndoto za mshambuliaji wa Mansfield Town ya Daraja la Pili England, Abdillah Yussuf ‘Adi’ kuichezea Taifa Stars kwa mara ya kwanza zimeyeyuka
Wachezaji waliokuwa kambini Taifa Stars chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco kwa maandalizi ya mchezo huo ni makipa; Shaaban Kado, Aishi Manula na Ally Mustafa ‘Barthez’.
Mabeki; Juma Abdul, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Kevin Yondan na David Mwantika.
Viungo; Ismail Khamis ‘Suma’, Said Ndemla, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Himid Mao, Mohammed Ibrahim, Ibrahim Hajib, Deus Kaseke, Farid Mussa na Shiza Kichuya.
Washambuliaji ni John Bocco, Thomas Ulimwengu, Nahodha Mbwana Samatta, Elias Maguri, Jeremiah Juma na Yussuf Adi.
Stars inashika nafasi ya tatu katika Kundi G, ikiwa na pointi nne baada ya kushinda mechi moja dhidi ya Chad, kufungwa na Misri 3-0 na kutoa sare ya 0-0 na Nigeria.
Misri inaongoza Kundi hilo kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na Nigeria yenye pointi tano. Misri na Nigeria wanarudiana Jumanne Cairo baada ya kutoa sare ya 1-1 Jumapili Kaduna.
MWADUI YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA TFF
Mwadui wametinga Nusu Fainali Kombe la TFF baada ya kuitoa Geita Gold |
MICHUANO
ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ngazi ya robo
fainali imeendelea leo kwa mchezo mmoja, ambapo Mwadui FC wameibuka na
ushindi wa mabao 3- 0 dhidi ya wneyeji Geita Gold FC.
Mchezo huo wa kwanza hatua ya robo fainali umechezwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, na Mwadui FC kujipatia mabao yake kupitia kwa Joram Mgeveke, Jeryson Tegete pamoja na Jabir Aziz ‘Stima’.
Baada ya ushindi huo Mwadui FC inasuburi kuungana na timu zingine tatu katika hatua ya Nusu Fainali ambayo michezo yake itachezwa mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu.
Michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho inatarajiwa kuendelea Machi 31 kwa michezo miwili, Yanga SC watakua wenyeji wa Ndanda FC uwanja wa Taifa mjini Dar es salaam, huku Azam FC wakiwakaribisha Tanzania Prisons katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Mchezo wa mwisho hatua ya nusu fainali utachezwa tarehe 7 April, ambapo Simba SC watakua wenyeji wa Coastal Union katika uwanja wa Taifa jijini Dar ess alaam.
Bingwa wa Kombe la Shirikisho atawakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.

Wababe wa Sudan wamtaka Elias Maguli kwa udi na uvumba
Uongozi wa klabu ya Al Hilal ambayo imekuwa ni moja ya timu zenye nafasi ya ‘kudumu’ katika hatua ya Nane Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika ulifadhaishwa mno na hatua ya kutolewa kwenye mashindano hayo msimu huu. Walitolewa na klabu ya Al Ahli Tripoli ya Libya na hivyo kufanya maamuzi magumu ya kuachana na wachezaji wake watatu wa kigeni, Abieku Ainosoon, Nelson Ladzagla, Souleymane Cisse.
Wakala wa Elias Maguli, Faustino Mukandila ambaye amekuwa akiwauzia wachezaji Al Hilal ameuambia mtandao wa Soka360 kuwa amefanya mazungumzo na rais wa wababe hao wa Sudan, Ashraf Al Kardinal kuhusiana na uhamisho wa Maguli.
Nashughulikia uhamisho wa Maguli kwenda Al Hilal kwenye dirisha la usajili lijalo mwezi wa sita. Wanahitaji sana huduma zake.Maguli amekuwa katika kiwango kizuri msimu huu tangu atue Stand United baada ya kuondoka Simba, amefunga mabao kumi mpaka sasa licha ya kuonekana kubaniwa na kocha wake Patrick Liewig.
Pia alikuwa ni moja ya wachezaji wa Tifa Stars waliong’ara kwenye mechi dhidi ya Algeria, akifunga bao moja Dar huku bao lake lingine likikataliwa kwenye mechi ya marudiano jijini Bilda.
STARS YAWASILI SALAMA,KUKIPIGA NA CHAD JUMATATU YA PASAKA
Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kimewasili Dar es Salaam usiku huu wachezaji wake wakiwa wamechoka baada ya safari ndefu tangu mchana kutoka D’jamena, Chad kupitia Addis Ababa, Ethiopia.
Mara baada ya kuwasili, Taifa Stars walipokewa na Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja ambaye aliwapa hotuba fupi ya mapokezi.
Stars ambayo Jumatano iliwafunga wenyeji Chad 1-0 katika mchezo wa Kundi G kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya mjini D’jamena mara baada ya kuwasili, ilikwenda moja kwa moja kambini, hoteli ya Urban Rose, katikati ya jiji.
Wachezaji waliowasili na Taifa Stars usiku huu kutoka Chad ni makipa; Aishi Manula na Ally Mustafa ‘Barthez’.
Mabeki; Juma Abdul, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Kevin Yondan na David Mwantika.
Viungo; Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Himid Mao, Mohammed Ibrahim, Ibrahim Hajib, Deus Kaseke, Farid Mussa na Shiza Kichuya.
Washambuliaji ni John Bocco, Thomas Ulimwengu na Nahodha Mbwana Samatta.
Wachezaji hao wataungana na wachezaji wengine sita waliobaki kambini Dar es Salaam, ambao ni kipa Shaaban Kado, viungo Ismail Khamis ‘Suma’, Said Ndemla na washambuliaji Elias Maguri, Jeremiah Juma na Abdillah Yussuf ‘Adi’.
Stars inashika nafasi ya tatu katika Kundi G, ikiwa na pointi nne baada ya kushinda mechi moja dhidi ya Chad, kufungwa na Misri 3-0 na kutoa sare ya 0-0 na Nigeria.
Misri inaongoza Kundi hilo kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Nigeria yenye pointi nne sawa na Tanzania, lakini ina wastani mzuri wa mabao, wakati Chad inashika mkia haina pointi.

Nahodha Mbwana Samatta akiwaongoza wachezaji wake kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam baada ya kuwasili usiku huu |
Wachezaji waliowasili na Taifa Stars usiku huu kutoka Chad ni makipa; Aishi Manula na Ally Mustafa ‘Barthez’.
Mabeki; Juma Abdul, Shomary Kapombe, Mwinyi Hajji, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Kevin Yondan na David Mwantika.
Viungo; Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Himid Mao, Mohammed Ibrahim, Ibrahim Hajib, Deus Kaseke, Farid Mussa na Shiza Kichuya.
Washambuliaji ni John Bocco, Thomas Ulimwengu na Nahodha Mbwana Samatta.
Thomas Ulimwengu akitoka Uwanja wa Ndege baada ya kuwasili |
Katibu wa BMT, Mohammed Kiganja akiwahutubia wachezaji Uwanja wa Ndege |
Wachezaji wa Taifa Stars wakimsikiliza Katibu wa BMT |
Wachezaji wa Taifa Stars wakimsikiliza kwa makini Katibu wa BMT |
Baadhi ya viongozi na wachezaz wakitoka Uwanja wa Ndege baada ya kuwasli |
Kutoka kulia ni Jonas Mkude, Aishi Mnula na Shiza Kichuya wakiwa Uwanja wa Ndege wa Addis Ababa, Ethiopia wakisubiri kuunganisha ndege ya kuja Dar es Saalaam |