WABUNGE wa Chama cha Wananchi
(CUF), wametangaza kuwaburuza mahakamani Ofisa mdhamini wa Vitambusho
vya Taifa vya Mzanzibari (ZAN-ID) Pemba, Hamadi Selemani na Ofisa
vitambulisho Wilaya ya Mkoani, Omar Ngwali.
Wamesema kuwa kusudio la kuwaburuza mahakamani maofisa hao ni kutokana na kuzuia haki ya kutowapa vitambulisho vya makazi watu 422, jambo ambalo linapelekea kushindwa kujiandikisha katika daftari la Tume ya Taifa Zanzibar (ZEC).
Kwa niaba ya wabunge na wawakilishi hao,
Mbunge wa Mkanyageni, Mohammed Habib Mnyaa, amesema walalamikiwa hao
wameshindwa kuwaandikisha wananchi hao katika daftari huku wakiendelea
kuwanyima vitambulisho vyao vya ZEC.
Mnyaa amesema “kutokana na kauli ya mkuu
wa wilaya, nawataka wabunge pamoja na wawakilishi kuwahamasisha wananchi
kujitokeza kwa ajili ya kujiandikisha katika daftari la kupiga kura.”
Amesema kutokana na kauli hiyo ya mkuu wa
wilaya, viongozi wengi pamoja na wabunge na wawakilishi waliamini kuwa
kuna uwezekano mkubwa wa kafanya hivyo.
“Sisi wabunge na wawakilishi
tuliwahamasisha wananchi kwenda mkoani kwa wingi kuchukua vitambulisho
kwa wale waliopiga picha na kuomba vitambulisho hivyo pamoja na wale
ambao vitambulisho vyao vya zamamani vimekwisha muda kupaswa kuchukua
vipya,”amesema.
Kwa kujibu wa kauli ya mkuu wa wilaya
katika kikao hicho, palikuwepo na vitambulisho zaidi ya elfu nne ambavyo
havijachukuliwa na wenyewe.
Mnyaa ameongeza kuwa, wabunge pamoja na
wawakilishi wakiwa wamefuatana na wananchi katika majimbo ambayo mara
kadhaa walikuwa wakienda mkoani –ofisi ya vitambulisho kwa kuchukua
vitambulisho vyao, lakini kwa makusudi walinyimwa na kuambiwa bado
havijafika.
Amesema kuwa wakati mwingine wananchi
walikuwa wakiambiwa kuwa uzalishaji wa vitatambulisho hivyo umesimama
kwa sababu ofisi ya vitambulisho Zanzibar hawakuingiziwa fedha kwa
mujibu wa bajeti yao waliyoomba na mara nyingine sababu ya vifaa vya
kuzalisha vitambulisho vimekwisha.
“Haya yote yakitokea kwa upande wa
wanachama wa CCM wao hakuna shida malalamiko yoyote na wakipiga picha
baada ya wiki mbili wanapatiwa vitambulisho vyao hata walio chini ya
umri wa miaka 18,” amesema Mnyaa.
0 comments:
Post a Comment