Home » » FELLAINI AIBEBA BELGIUM, COUTINHO BRAZIL!

FELLAINI AIBEBA BELGIUM, COUTINHO BRAZIL!


FellainivArsenal
 Kwenye Mechi za Kimataifa za Kirafiki zilizochezwa Jana, Wachezaji wa Ligi Kuu England, Marouane Fellaini na Philippe Coutinho, waliwika na kuzisaidia Nchi zao kupata ushindi.
Huko Stade de France Jijini Paris, Belgium imekuwa Nchi ya Kwanza kuibamiza France Bao 4 Uwanjani kwao waliposhinda 4-3.
Bao za Mechi hiyo zilifungwa na Fellaini, Bao 2, Radja Nainggolan na Penati ya Eden Hazard kwa Belgium na zile za France kufungwa na Mathieu Valbuena, Penati, Nabil Fekir na Dimitri Payet.
Fowadi wa Arsenal, Olivier Giroud, alianza Mechi hii badala ya Majeruhi Karim Benzema lakini alishindwa kumsumbua Kipa wa Belgium, Thibaut Courtois, anaedakia Chelsea.
Wakati France ndio Wenyeji wa Fainali za EURO 2016, Belgium Ijumaa watapambana na Wales katika Mechi ya Kundi B la kufuzu EURO 2016.
BRAZIL 2 MEXICO 0
Huko Sao Paulo, Brazil, wakicheza Mechi yao ya kwanza Nchini kwao tangu Mwaka Jana wafedheheshwe kwenye Fainali za Kombe la Dunia, waliitandika Mexico Bao 2-0.
Bao zote za Brazil zilifungwa Kipindi cha Kwanza na Philippe Coutnho wa Chelsea, likiwa Bao lake la kwanza kwa Nchi yake, na Diego Tardelli.
Huu ni ushindi wa 10 kwa Brazil chini ya Kocha Dunga alietwaa wadhifa mara baada ya Kombe la Dunia kwa kumrithi Luiz Felipe Scolari.
Jumatano Brazil itacheza tena Kirafiki huko Porto Allegre Nchini Brazil na Honduras na kabla kwenda Chile kushiriki Copa America.
VIKOSI;
BRAZIL-Jefferson, Danilo, David Luiz, Filipe Luis, Miranda, Elias, Fernandinho, Fred, Coutinho, Willian, Diego Tardelli
MEXICO-J. Corona, Aldrete, Corral, Hugo Ayala, Dominguez, Rafa Marquez, Guemez, Corona, Osuna, Herrera, Jimenez
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger