Home » » RUSSIA NA QATAR KUPOKWA UENYEJI WA KOMBE LA DUNIA

RUSSIA NA QATAR KUPOKWA UENYEJI WA KOMBE LA DUNIA


 
 
Mkuu wa kamati ya ukaguzi wa fedha na uchunguzi ya FIFA, DOMENICO SCALA
 
Katika hatua nyingine Hofu imetanda kuwa huenda nchi za RUSSIA na QATAR zikapokwa uwenyeji wa fainali za kombe la FIFA la dunia mwaka 2018 na 2022 iwapo ushahidi wa kuwepo kwa vitendo vya rushwa utapatikana dhidi yao.

Mkuu wa kamati ya ukaguzi wa fedha na uchunguzi ya FIFA, DOMENICO SCALA ameliambia jarida moja la USWISI, SONNTAGSZEITUNG, kuwa haki ya kuandaa fainali hizo za kombe la FIFA la dunia huenda ikapokwa kutoka kwa URUSI na QATAR iwapo kutakuwepo na ushahidi kuwa nchi hizo zilitoa rushwa kupata kandarasi hiyo ya uenyeji.

Hata hivyo SCALA amekanusha kuwa hadi sasa amepata wala kuona ushahidi wa aina yeyote dhidi ya mataifa hayo mawili.

FIFA inakumbwa na mgogoro wa kukamatwa kwa maafisa wake kutokana na tuhuma na mashtaka ya ulaji rushwa ikiwa ni miongoni mwa mashtaka yaliofunguliwa na MAREKANI.

Kwa sasa uchunguzi unaendelea juu ya tuhuma za rushwa ndani ya FIFA ambapo kitengo maalumu cha makosa ya jinai nchini USWISI kimelivalia njuga suala hilo.
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger