WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick
Sumaye, amekitahadhalisha Chama cha Mapinduzi (CCM), kuacha kuteua
mgombea Urais, ambae anatumia fedha kuwahonga wananchi ili wamchague
katika uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Sumaye amesema endapo chama chake kitamteua mgombea urais ambae ni mtoa rushwa na muabudu rushwa, atakihama chama hicho na kwamba hatakubali kuona jina lake linakatwa kirahisi na akaendelea kuvumilia.
Sumaye ametoa kauli hiyo wakati
akizungumza na waandishi wa habari mkoani Shinyanga, ambamo amesema
endapo atakatwa jina lake kiharari na mgombea kuteuliwa ambae sio
muabudu rushwa atakuwa tayari kusaidiana nae.
Amesema kuwa baadhi ya wagombea
waliotangaza kuwania urais kupitia chama hicho, wengine kanuni
haziwakubalibali bali wanasindikiza wenzao katika kinyang`anyiro hicho
hivyo ana imani ataibuka kidedea.
“Watia nia 34 waliotangaza mpaka sasa,
wapo wengine ambao hawaitaji urais na wala kanuni za chama chetu
haziwakubali hao wanasindikiza wenzao, hao tayari wameishajitoa wenyewe
na siwafikirii”.amesisitiza Sumaye
Hata hivyo amesema chama hicho kinapaswa
kuteua mtu ambae ni msafi asiekuwa na kashfa yeyote atakaesababisha
chama hicho kushindwa kutwaa dola katika uchaguzi mkuu wa Oktoba Mwaka
huu.
Amesema umefika wakati wa CCM kutafakari
na kuchuja watangaza nia waliojitokeza hata wale ambao wanasindikiza
wenzao katika safari hiyo, ili kutoa mtu ambaeambae ana nia thabiti
kuwatumikia wananchi.
Ameongeza uchaguzi huu utakuwa na
vitimbwi na vituko vya kila aina hivyo watanzania wanapaswa kuwa
watulivu katika kufanikisha kumpata kiongozi ambae ni bora na muadilifu.
Amesema vyama vya siasa nchini vinapaswa
kutoa maelekezo mazuri kwa wananchama na wafuasi wao ili kuepusha vurugu
zisizokuwa za lazima katika uchaguzi huo na nkutetea maslahi ya umma.
“Siasa ni hoja na wala siasa sio kutumia
nguvu, nondo, risasi, rungu na panga ili kuingia ikulu, hapana ni
kutumia hoja nzuri na kuwaelimisha wafuasi katika kufanya mambo ambayo
ni mazuri,” amesema Waziri huyo wa zamani.
0 comments:
Post a Comment