Jeshi la
polisi wilayani Iramba limetumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha
kuwatawanya wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na
kuwakamata Mwenyekiti wa uhamashishaji kanda ya kati Bi Jesca Kishoa na
katibu wa BAVITA wilayani Iramba Bwana Rayman Minja, wakati walipokuwa
wakiwahamasisha wananchi kwenye mkutano wa hadhara kujiandikisha kwenye
daftari la kudumu la wapiga kura. ,
Akieleza
baada ya kuachiwa na jeshi la polisi alipokuwa amewekwa chini ya usalama
kwa zaidi ya masaa matano mwenyekiti wa uhamashishaji CHADEMA kanda ya
kati Bi. Jesca Kishoa, amesema anashangaa kuona Mkuu wa Wilaya ya Iramba
akiwakataza kufanya mikutano huku vyama vingine vimekuwa vikifanya
mikutano, jambo ambalo hastahili kufanya hivyo kwa sababu yeye anatawala
wananchi wenye vyama tofauti na siyo chama kimoja.
Kwa
upande wao, wananchi wa wilaya ya Iramba wametupia lawama kwa jeshi la
polisi kuzuia mikutano minne ya CHADEMA, pia kutumia nguvu kutawanya
watu kwa kuwa mwagia maji ya kuwasha na kuwapiga mbomu ya machozi.
Akionge
kwa simu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida, Bwana Thobias
Sedoyeka amesema wao wanatekeleza amri ya Mkuu wa Wilaya ya Iramba ya
kupiga marufuku na kuzuia mikutano yoyote ya hadhara ifanyike wilayani
humo.
Taarifa via ITV
0 comments:
Post a Comment