SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini
TFF leo limezindua jezi mpya za timu za Taifa, zitakazokuwa zikitumika
na timu za Taifa katika michuano mbali mbali itakayokua inazikabili.
Uzinduzi huo wa jezi mpya uliofanyika
katika ukumbi wa Kilimanjaro jengo la Golden Jubilee uliambatana na
uziduzi wa tovuti mpya ya shirikisho, uliongozwa na mgeni rasmi Mh. Said
Mtanda, mbunge wa jimbo la Mchinga na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Maendeleo ya jamii.
Katika uzinduzi huo, kulizunduliwa jezi
aina tatu, ambazo ni jezi za ugenini, jezi za nyumbani na jezi
zitakazokuwa zikitumika kwa ajili ya mazoezi.
WATANZANIA SABA WATEULIWA KAMATI ZA CAF
Shirikisho la mpira barani Afrika CAF
limewateua watanzania saba kuwa wajumbe wa kamati zake mbali mbali kwa
kwa kipindi cha miaka miwili 2015-2017.
Walioteuliwa pamoja na kamati zao katika mabano ni:
1. Leodeger Tenga- (Makami Mwenyekiti
Kamati ya Fedha, Mjumbe wa Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya fainali za
Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa ndani (CHAN), Mwenyekiti wa Kamati ya
Mpira wa Wanawake, na Mjumbe wa Kamati ya Vyama Wanachama).
2. Jamal Malinzi – (Mjumbe kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya miaka 20)
3. Mwesigwa Selestine – (Mjumbe Kamati ya Uendeshaji Mashindano ya Vijana Umri chini ya Miaka 17).
4. Richard Sinamtwa -(Mjumbe Kamati ya Rufaa)
5.Dr Paul Marealle -(Mjumbe Kamati ya Tiba)
6. Lina Kessy -(Mjumbe ya Soka la Wanawake)
7. Crescentius Magori-(Mjumbe Kamati ya Soka la Ufukweni na Soka la Ndani)
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania –
TFF linawapongeza wajumbe wote walioteuliwa kuingia katika kamati mbali
mbali na linawatakia kila la kheri wanapoiwakilisha nchi yetu.
0 comments:
Post a Comment