Zipo ripoti nzito toka England zinazodai Meneja wa Manchester United Louis van Gaal na Kipa wa Tottenham Hugo Lloris
wamefikia muafaka na Kipa huyo wa Kimataifa wa France ambae
ameshakubaliana kuhusu maslahi yake binafsi huko Old Trafford.
Huku kukiwa na mipango ya chini chini ya Kipa Nambari Wani David de
Gea kurudi kwao Spain kuidakia Real Madrid, kumchukua Hugo Lloris
kunaelekea kuziba pengo hilo.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi, Gazeti linaloheshimika huko
France L'Equipe, kilichobaki sasa ni mazungumzo ya kukubaliana Ada ya
Uhamisho na Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy.
L'Equipe imedai Levy amemhakikishia Lloris kuwa Klabu yeyote
itakayotoa Ofa ya Pauni Milioni 18 kwenda juu basi atamruhusu kuhama
White Hart Lane.
Lloris, mwenye Miaka 28, alijiunga na Tottenham Mwaka 2012 akitokea Lyon ya France kwa Dau la Pauni Milioni 11.4.
Hata hivyo, Levy anasifika mno kwa ugumu wa kutoa Wachezaji wake Nyota na kama akiwaruhusu basi Dau lao huwa sio masihara.
0 comments:
Post a Comment