Kabla ya polisi kuchukuwa hatua hiyo wanafunzi hao walifanya
maandamano ndani ya chuo hicho huku wakiimba nyimbo mbalimbali za
mashinikizo na wakiweka kambi nje ya jengo la utawala hali
iliyosababisha uongozi wa chuo kufunga chuo kwa muda usiojulikana na
kuwataka waondoke bila mafanikio.
Hata hivyo baada ya muda mfupi magari ya polisi yaliongezeka yakiwa
na polisi waliokuwa na mabomu ya machozi na silaha za moto na baadae
gari la maji ya kuwasha likawasili na hapo ndipo vurugu zikaanza wakati
polisi wanawamwagia maji ya kuwasha wakaanza kurusha mawe, mabomu ya
machozi yakafuatia hali iliyopelekea wanafunzi kadhaa kujeruhiwa na
wengine kukamatwa na polisi.
Mara baada ya sakata hilo kiongozi wa wanafunzi wanaosoma kozi ya
famasia Bw.Levid Pavela akazungumza na waandishi wa habari ambapo
amesema mgomo huo ni mara ya tatu na ulitokana na baadhi ya wanafunzi
waliohitimu kozi hiyo kushindwa kuajiriwa kwa madai haitambuliki na bodi
ya famasia huku akizungumzia tukio hilo.
Akizungumzia suala hilo naibu mkurugenzi wa kitengo cha udahili wa
chuo hicho Bw. Lotha Samora amekiri kuwa bado hawajapata usajili wa kozi
hiyo na kuongeza kuwa walishapeleka maombi bodi ya Famasia tangu mwaka
2011 lakini hadi leo hawajafanikiwa.
0 comments:
Post a Comment