Timu ya soka ya Newcastle United imemtimua kocha wake mkuu John Carver pamoja na msaidizi wake Steve Stone.
Carver mwenye umri wa miaka 50 alichukua nafasi ya kocha Alan Pardew aliyetimkia timu ya Crystal Palace.Katika michezo ishirini aliyoiongoza timu hiyo alifanikiwa kushinda michezo mitatu.
Mkurugenzi mkuu wa timu hiyo Lee Charnley, amesema atatafutwa kocha mpya wa kuweza kuijenga timu hiyo upya.
Kumekua na tetesi kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Uingerza Steve McClaren, anaweza kuchaguliwa kuwa kocha mpya wa kikosi cha Newcastle United.
0 comments:
Post a Comment