KATIKA jitihada za kuinua ubora wa
elimu ya ufundi nchini, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE)
limevifutia usajili vyuo vitatu na kuvishushia hadhi vyuo 16
Vyuo hivyo ambavyo vimefutiwa usajili ni Dar es Salaam College of Clinical Medicine kilichokuwa na usajili wa awali, Ndetele School of Medical Laboratory Sciences, na Institute of Information Teknology vyote vya Dar es Salaam.
Vilivyoshushwa hadhi ni pamoja na Sura
Technologies- Dar, Institute of Management and Information Technology-
Dar, Techno Brain- Dar, Ministry of Agricukture Training Institute
Igurusi- Mbeya, Mbozi School of Nursing -Mbeya, KCMC AMO Ophthalmology
School- Moshi, KCMC AMO Anaesthesia School -Moshi.
Vingine ni Advanced Pediatrics Nursing
KCMC Moshi, AMO Training Centre Tanga, CATC Songea, CATC- Sumbawanga,
COTC Maswa- Shinyanga, COTC -Musoma, Dentak Therapists Training Centre-
Tanga, Ndudu School of Environmenta- Kwimba na KCMC AMO General School
Moshi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo
Jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa NACTE, Dkt. Adolf
Rutayuga amesema kuwa, hatua hizo zimefikiwa baada ya vyuo vingi
kushindwa kurekebisha kasoro zilizobainishwa na NACTE.
“Kwa kutumia sheria za Bunge sura Na.129
na kanuni za Baraza za usajili (2001), 20 Februari 2015, baraza lilitoa
notisi ya siku 30 kwa Taasisi na vyuo vya umma. Notisi ililenga kuzipa
taasisi na vyuo nafasi ya kujitetea na kufanya marekebisho ya makosa
yaliyobainishwa,” amesema Rutayuga.
Amesema, kunabaadhi ya vyuo ambavyo
vilivyofanyia kazi upungufu wao baada ya notisi kutolewa lakini kuna
vingine vilikaidi maagizo hayo, hivyo havikuchukua hatua yoyote.
Aidha, baraza limechukuwa hatua hizo kwa mujibu wa sheria na kanuni zake ambapo walibaini makosa yafuatayo;-
Kumalizika kwa muda wa usajili wa awali,
kutoanza mchakato wa kupata ithibati baada ya kupata usaili kamili,
kumalizika kwa muda wa ithibati, kutochukua hatua ya kuomba upya
ithibati na vyuo kuamua vyenyewe kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu
mbalimbali.
Hata hivyo Rutayuga amesema, wanafunzi
ambao wapo katika vyuo vilivyofutiwa usajili watapatiwa ufumbuzi na
kupelekwa kwenye vyuo vyenye usajili kupitia NACTE.
Rutayuga ametoa wito kwa wazazi pamoja na
wanafunzi kuvichunguza vizuri vyuo kabla ya kujiandikisha ili kuepuka
matatizo na uzembe unaofanywa na uongozi wa chuo husika.
0 comments:
Post a Comment