Ripoti hii ni ya ITV June 27 2015
kutoka Morogoro inahusu watu watatu kufariki katika mapambano na
Polisi, huku wawili kati yao wakihisiwa kuwa na uhusiano na kundi la
kigaidi la Al Shabaab.
Breaking News nyingine kuhusu tukio hilihili iliyoripotiwa na Gazeti la Mwananchi inahusu
watu sita kukamatwa na wengine 50 wanatafutwa, walikutwa wakiwa na sare
za majeshi pamoja na silaha kama majambia kwenye msitu Mvomero.
Kwenye taarifa iliyofatia kutoka
Mwananchi, imesema Mkulima Cassian Peter amefariki mchana wa June 27
2015 kwenye Hospitali ya Bwagala ambapo Polisi mmoja amelazwa na hii ni
baada ya kujeruhiwa na hao watuhumiwa wa Ugaidi kabla hawajakamatwa.
Mtangazaji na Mwandishi wa habari wa Radio One Maulid Kambaya kwenye page yake ya Facebook alipost picha za walivyokamatwa navyo ‘Magaidi’ hawa.
Jiunge na mimi
0 comments:
Post a Comment