KUNDI la vijana waporaji maarufu
kama “Panya Road” linadaiwa kuvamia eneo la Tabata jijini Dar es Salaam
na kuwashambuli watu kwa mapanga na nondo kisha kuwapora fedha na simu
katika mitaa ya Kimanga na Kisukuru.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilala, Lucas Mkondya, alipotakiwa kuthibitisha tukio hilo, alikiri kuwa na taarifa hizo lakini akasema hawezi kuzungumza na mwandishi kwenye simu.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, hakuweza kupatikana katika simu yake ya kiganjani.
Kwa mujibu wa walioshuhudia tukio hilo,
amesema lilitokea saa 11 jioni jana ambapo wananchi waliporwa mali zao
kabla ya askari polisi waliokuwa doria kuzima tukio hilo.
“Hilo kundi lilikuwa vijana wengi
wametusumbua sana maeneo ya Tabata na kuwapora watu vitu vyao, ukiwa
mbishi unakatwa mapanga,”amesema shuhuda huyo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, “Panya Road”
hao walikuwa wakilipiza kisasi baada ya mwenzao kuuliwa na wananchi
wenye hasira baada ya kumuibia mteja simu katika klabu moja maarufu
iliyoko maeneo ya Tabata.
0 comments:
Post a Comment