Home » » DANGOTE ALIDHIA UJENZI WA BANDARI YAKE MTWARA

DANGOTE ALIDHIA UJENZI WA BANDARI YAKE MTWARA




 Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Hawa Ghasia alipowasili kwenye uwanja wa Ndege mjini Mtwara jana kwa ajili ya kutembelea kiwanda chake cha Cementi kilichoko Msijute, mkoani Mtwara.

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Hawa Ghasia akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Mtwara leo kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha Cementi cha Dangote. Katikati ni Balozi wa Nigeria Nchini Tanzania, Ishaya Manjanbu.(P.T)


 Mkurugenzi wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote (kulia), akijadiliana jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka, walipokutana mjini Mtwara jana kuangalia uwezekano wa kujenga kituo cha kusafirisha saruji katika eneo la Bandari ya Mtwara.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, akizungumza na waandishi wa habari baada kuwasili mjini Mtwara jana na kutembelea kiwanda chake cha Cementi, kilichoko Msijute, mkoani Mtwara.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote akisaini kitabu cha wageni, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege mjini Mtwara jana, kwa ajili ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda chake cha saruji. Kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka.

 Mkurugenzi wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote akiwafuatana na wenyeji wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Hawa Ghasia (wa pili kushoto), Balozi wa Nigeria, Ishaya Manjanbu (wa pili kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Bi. Fatma Salum Ali (kushoto), alipowasili kwenye uwanja wa ndege, mjini Mtwara jana.





Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Dangote, Alhaj Aliko Dangote, akiteta jambo na Mwakilishi mkazi wa Dangote nchini Tanzania, Bi. Esther, mjini Mtwara , baada ya Mkurugenzi huyo kutembelea kiwanda chake cha saruji kinachojengwa mkoni Mtwara.

 

    Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

    0 comments:

     
    Supported by AMAGA Media services : | |
    Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
    Templete Designed by Abdallah Magana
    Proudly powered by Blogger