Home » » KUELEKEA COPA AMERICA: AGUERO, DI MARIA, FALCAO HATARI MECHI ZA KIRAFIKI.

KUELEKEA COPA AMERICA: AGUERO, DI MARIA, FALCAO HATARI MECHI ZA KIRAFIKI.

COPA-AMERICA15Copa America, Kombe la Mataifa ya Marekani ya Kusini, linaanza Nchini Chile Wikiendi ijayo na Nchi hizo zipo kwenye matayarisho makali huku Mabingwa Watetezi Uruguay wakiiadhibu Guatemala 5-1 na Argentina kuwawasha Bolivia 5-0

Uruguay, wakicheza bila ya Luis Suarez ambae yuko Kifungoni na pia alikuwa huko Berlin kuichezea Barcelona kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, waliichapa Guatemala Bao 5-1 kwa Bao za Diego Rolan, Edinson Cavani, Bao 2, Giorgian De Arrascaeta na Abel Hernandez.
Uruguay watafungua utetezi wa Taji lao la Copa America huko Nchini Chile kwa kucheza na Jamaica Juni 13 na kisha kucheza na Argentina na Paraguay katika Mechi za Kundi B.
Hata hivyo, Uruguay hawawezi kumtumia Luis Suarez ambae anatumikia Kifungo cha Mechi 9 kwa kumng'ata Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini Mwaka Jana kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.
Nao Argentina, wakicheza bila ya Lionel Messi, Javier Mascherano na Carlos Tevez, ambao walikuwa wakichezea Klabu zao kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI wakati Barcelona wakicheza na Juventus huko Berlin, waliinyuka Bolivia Bao 5-0 huko Estadio San Juan del Bicentenario Mjini San Juan.
Bao za Argentina zilipigwa na Sergio Aguero, Bao 3, na Angel Di Maria Bao 2.
Nako huko Diego Armando Maradona Stadium Mjini Buenos Aires Nchini Argentina, Radamel Falcao alifunga Bao la ushindi wakati Colombia inaitungua 1-0 Costa Rica.
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger