Ndani
ya wiki moja baada ya Serikali ya Marekani kupitisha Sheria ya kuruhusu
Ndoa za jinsia moja kwa raia wake kumekuwepo na maoni mbalimbali kutoka
kwa watu kuhusiana na maamuzi hayo.
Mmoja wa watu walioguswa na maamuzi hayo ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabeambaye ameeleza hisia zake baada ya maamuzi hayo kupitishwa.
Rais wa Marekani Barack Obama
Katika mahojiano na radio ya Taifa ya Zimbwabwe, Mugabe alisema
hawezi kupingana na maamuzi ya nchi hiyo kwani ni sheria ambayo
imepitishwa na Serikali na kama ni hivyo ataamua kufunga safari kwenda
mpaka Washington kuomba kufunga ndoa na RaisBarack Obama.
Ameongeza
kuwa, Serikali ya Marekani imekuwa ikiongozwa na wajinga ambao ni
wafuasi wa shetani wanaoitukana taifa la Marekani akisisitiza Marekani
imechafuka na wanaiendesha nchi kwa dhana zao binafsi ambazo ni potofu
Kim Kardashian ni
mwanadada ambaye anajulikana kwa kutengeneza headlines nyingi sana na
moja kati ya headlines anazoziweka public personality huyu ni zile
zinazohusu uzuri wake. Lakini Kim anasema
amechoshwa na fikra za watu wengi wanaodhani kuwa yeye ni mwanamke
mzuri tuu asiye na akili ya kufikria mbali, na kwa sababu hiyo staa huyu
ameweka headlines nyingine kubwa, ametangaza kurudi shule!
Kim Kadarshianamesema
anahisi yeye kama mtu binafsi hana uwezo mkubwa wa kutosha
kiakili. Licha ya mamillioni na umaarufu wote alionao sasa hivi, Kim
ameamua kurudi shule kupanua IQ huku akidai IQ yake haiko kwenye levo
anayoitaka na anaona bora arudi kusoma, ameshapata umaarufu na pesa yupo
tayari kuwekeza nguvu zake kwenye vitu vingine anavyoona ni muhimu na
mume wake Kanye West amekua akimsisitiza Kim kujaribu vitu tofauti haswa kipindi hiki ambacho ana mimba.
Lakini kumekuwa na baadhi ya watu wanaohisi kuwa jambo hili sio la ukweli na Kim anataka kupata watazamaji wengi zaidi wa Tv reality show yake Keeping up with The Kadarshians lakini msemajiwa
Kim amepinga maneno haya na kusema kuwa staa huyo yupo serious na
kurudi kusoma, na yeye kupata watazamaji wengi zaidi haiusiani ya
maamuzi yake binafsi. Kwenye interview aliofanya, staa huyo alisema;
>>>“Nahisi
nishafanikisha lengo la kuwa maarufu na tajiri, kwa kipindi cha zaidi
ya miaka kumi na kitu hilo ndio lilikua lengo langu, likatimia,
nikajulikana, nikawa tajiri, nikaolewa na kuzaa mtoto wangu wa kwanza na
sasa nategemea mtoto wa pili, nahisi umefika wakati wa mimi kurudi
kusoma”. >>>Kim Kadarshian.
Msemaji mkuu wa Kim Kadarshian amesema
kwa sasa wanaangalia namna ya kufanikisha zoezi la yeye kupata vipindi
maalum nyumbani kwake kwa ushirikiano wa mwalimu atakayekuwa tayari
kumsaidia kufanikisha lengo hili.
Katibu
wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Kulwa Milonge, akionyesha fomu zenye
orodha ya majina ya wanachama wa ccm,104,03 waliomdhamini kugombea
urais, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa(kulia). Mwenyekiti
Mstaafu wa CCM Mkoa wa Morogoro, Kanali Mstaafu, Isaac Mwasongo,
akisindikiza na Mwanasiasa Mkongwe, Steven Mashishanga(kushoto) baada ya
kuzngumza katika mkutano wa Waziri Mkuu wa zamani,Edward Lowassa, wa
Mkoa wa mwisho wa kupokea majina ya wadhamini kugombea urais
Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akizungumza na wanachama wa CCM na
wananchi wa Mkoa wa Morogoro jana wakati wa akitoa shukrani katika
kuhitimisha Mkoa wa mwisho wa kupokea orodha ya majina ya wadhamini wa
kugombea urais
Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter amekariri kuwa hakujiuzulu kama rais wa shirikisho hilo.
Kiongozi huyo mswissi mwenye mri wa miaka 79 alikuwa amedhaniwa
kujiondoa madarakani juni tarehe 2 kufuatia kashfa kubwa ya ufisadi
ulajirushwa na matumizi mabaya ya madaraka iliyokumba shirikisho lake
lakini sasa anaonesha dalili za kubadili mtazamo huo.
Blatter
ambaye ameiongoza FIFA kwa miaka 17 alikuwa ametangaza kuwa atajiondoa
mbele ya kamati kuu ilikufanyike uchunguzi wa kina katika FIFA lakini
sasa ameikumbusha jarida moja la uswisi BLICK kuwa yeye ndiye rais wa
FIFA na kuwa aliweka hatima yake mikononi mwa kamati kuu ya shirikisho
katika mkutano wa dharura.
Blatter anadhaniwa kuwa anafikiria kuwania tena uongozi wa shirikisho hilo.
Tuhuma
za udhabirifu wa fedha ufisadi na ulaji rushwa ulianza katika ileile
wiki ambayo Blatter alichaguliwa ikiendeshwa na Marekani.
Lakini
punde baada ya uchaguzi utawala nchini Uswisi nao ukaanzisha uchunguzi
sambamba wa ulaji rushwa na ufisadi dhidi ya maafisa wakuu katika
shirikisho la soka duniani FIFA.
Blatter alitangaza kuwa
anajiondoa uongozini ilikuruhusu uchunguzi ufanyike siku nne tu baada ya
kuchaguliwa upya kwa hatamu ya uongozi wa FIFA.
Kufuatia uchunguzi unaoendelea hakuna mipango na dalili zozote kuwa Blatter ama katibu mkuu wa FIFA
Jerome Valcke atakuwa mjini Ontario Canada katika fainali ya kombe la dunia kwa wanawake.
Kwa
kawaida Blatter angekuwa huko ilikutoa zawadi ya kombe la dunia kwa
timu itakayoibuka mshindi lakini hadi kufikia sasa hakuna mipango
yoyote ya ziara hiyo.