Louis
van Gaal amekiri Javier Hernandez 'Chicharito' atapata nafasi nyingine
ya kupigania nafasi yake kwenye Kikosi cha Manchester United akiungana
na Timu hiyo hapo Julai 25 huko Ziarani Marekani.
Chicharito, ambae aliifungia Man United Bao 59 katika Mechi154,
alipelekwa kwa Mkopo huko Real Madrid Msimu uliopita baada Van Gaal
kuamua atakuwa nyuma ya Wayne Rooney, Robin van Persie na Radamel Falcao
katika kupewa namba.
Lakini, baada ya Man United kuifunga Club America 1-0 mapema Leo,
Van Gaal aliulizwa hatima ya Chicharito na kueleza: "Chicharito anakuja
Julai 25. Ana nafasi ya kudhihirisha uwezo wake hasa baada ya Falcao na
Van Persie kuondoka, hivyo nafasi yake kubwa."
Hivi sasa Man United imebakiwa na Mastraika Wawili tu
wanaotambulika ambao ni Kepteni Wayne Rooney na James Wilson na
alipoulizwa kuhusu upungufu huo, Van Gaal alijibu: "Hapana tunae Rooney
anaweza kucheza kama Straika mkuu. Wanahabari wote Msimu uliopita
waliandika anapaswa kucheza hapo na mimi nawasikiliza. Na tunae
Chicharito, na labda Wilson, na pengine kwa kushangaza..mpya., huu ni
mchakato. Sina wasiwasi na nafasi hiyo."
0 comments:
Post a Comment