JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
RPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572
S. L. P. 260,
Fax - +255252503734
MBEYA.
E-mail:- rpc.mbeya@tpf.go.tz
tanpol.mbeya@gmail.com
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS
RELEASE” TAREHE 03.07.2015.
·
WATU WAWILI WA FAMILIA MOJA AUAWA KWA KUPIGWA
FIMBO WILAYANI CHUNYA.
·
MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO AFARIKI DUNIA PAPO
HAPO BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA
WAHAMIAJI HARAMU 13 RAIA WA NCHINI BURUNDI.
·
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU
MMOJA MKAZI WA KILOMBERO – MOROGORO AKIWA NA MILIPUKO [FATAKI] 78 BILA KIBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU WAWILI WA
FAMILIA MOJA WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1.
YUNGE DOTTO (45) [MAMA ] NA 2. MAHONA
ROBERT (16) [MTOTO] WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA TOTOE WALIUAWA KWA KUPIGWA
FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO NA ROBERT
MAKENZA (49) MKAZI WA KIJIJI CHA TOTOE [BABA] WA FAMILIA HIYO.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.07.2015
MAJIRA YA SAA 02:00 USIKU HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA MWAWADIMI, KIJIJI CHA IYOVYO, KATA YA TOTOE, TARAFA YA
SONGWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA,
CHANZO CHA TUKIO HILO NI MGOGORO WA KIFAMILIA BAADA YA MTUHUMIWA [BABA WA
FAMILIA HIYO] KUITUHUMU FAMILIA YAKE KUMUOZESHA/KUMTOROSHA BINTI YAKE AITWAE KWANGU ROBERT (17) MKAZI WA TOTOE KWA
MWANAUME KATIKA KIJIJI CHA MPONA.
AIDHA KATIKA
TUKIO HILO, WATOTO WENGINE SITA WA FAMILIA HIYO WALIJERUHIWA NA WAMELAZWA KITUO
CHA AFYA MBUYUNI KWA MATIBABU. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO NA
JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WANAFAMILIA KUTATUA MIGOGORO YAO YA KIFAMILIA KWA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO
ILI KUFIKIA MUHAFAKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI
ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA KWA HATUA ZAIDI ZA
KISHERIA.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAFUNZI WA
DARASA LA TANO KATIKA SHULE YA MSINGI IDWELI ALITAMBULIKA KWA JINA LA TUMAIN EXAUD (16) ALIFARIKI DUNIA PAPO
HAPO BAADA YA KUGONGWA NA PIKIPIKI YENYE NAMBA ZA USAJILI T.888 ABC AINA YA KINGLION
ILIYOKUWA IKIENDESHWA NA NZONGWA MBWILE
(26) MKAZI WA IDWELI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 02.07.2015
MAJIRA YA SAA 15:00 ALASIRI HUKO
KATIKA KIJIJI CHA IDWELI, KATA YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE,
MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA KUU YA MBEYA/TUKUYU.
CHANZO CHA AJALI
NI MWENDO KASI, MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA UPELELEZI UNAENDELEA.
TAARIFA ZA MISAKO:
KATIKA
MSAKO WA KWANZA, JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA
NDAHISHIMEYE JACRINE (34) MTUSI,
MKAZI WA MAKAMBA – NYANZARI NCHINI BURUNDI NA WENZAKE 12 WAKIWEMO WATOTO WENYE UMRI KATI YA MIAKA 11/2 HADI
MIAKA 15 WAPATAO 10 WOTE RAIA NA
WAKAZI WA NCHINI BURUNDI WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
WAHAMIAJI HAO
WALIKAMATWA MNAMO TAREHE 02.07.2015
MAJIRA YA SAA 17:30 JIONI HUKO VWAWA
MJINI, KATA NA TARAFA YA VWAWA, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA,
WAHAMIAJI HAO WALITOROKA KUTOKA KATIKA KAMBI YA ZEREKA – LILONGWE NCHINI MALAWI
KWA MADAI YA HALI MBAYA YA HUDUMA HUSUSANI CHAKULA NA WALITOKA NCHINI KWAO
BURUNDI MWAKA 2013 KUTOKANA NA MACHAFUKO. TARATIBU ZA KUWAKABIDHI IDARA YA
UHAMIAJI KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZINAENDELEA.
KATIKA MSAKO WA PILI:
JESHI LA POLISI
MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KILOMBERO MKOANI MOROGORO
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ATSON MUBWA
(50) BAADA YA KUKAMATWA AKIWA NA MILIPUKO [FATAKI] 78 ZILIZOTENGENEZWA KIENYEJI BILA KIBALI.
MTUHUMIWA
ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 01.07.2015
MAJIRA YA SAA 17:15 JIONI HUKO
KATIKA STESHENI YA TRENI – TAZARA – IYUNGA, KATA NA TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA
MKOA WA MBEYA AKIWA KWENYE BEHEWA K2
NAMBA 3051 AKIWA NA TIKETI YA
KUSAFIRIA YENYE NAMBA 00221 KUTOKA
DSM – CTA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA ZA MTU/WATU AU KIKUNDI CHA WATU
ANACHOKITILIA MASHAKA KATIKA MAENEO YAO ILI UCHUNGUZI NA HATUA ZAIDI ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
0 comments:
Post a Comment