Watu waliokisiwa kuwa majambazi wamekivamia kituo cha polisi Stakishari ukonga. Kwa mujibu wa taarifa za awali watu hao inasemekanaya wamevunja store ya silaha na kuchukua silaha zote aina ya SMG zilizopo kituoni hapo….hadi sasa inasemekana kuna vifo vya polisi ambao idadi yake haijajulikana wameuwawa na pia kuna jambazi mmoja aliyepigwa na risasi ya jambazi mwenzie….Jambazi huyo aliyeuwawa inasemekana ni dereva wa bodaboda wa kituo cha Nji Panda aliyefahamika kwa jina la Madevu.
Taarifa hizo zinasema majambazi
hayo yametokomea na kuacha pikipiki 3….hali si shwari mitaa ya
Stakishari na maeneo ya karibu baada ya milio ya bunduki kutawala maeneo
yote. watu walio wengi wamejifungia majumbani mwao na sasa hivi kelele
za ving’ola vya magari ya polisi vinasikika Stakishari maeneo
yote……kwa habari zaidi tuendelee kufuatilia
0 comments:
Post a Comment