Meneja mpya wa Real Madrid Rafael Benitez ametoboa kuwa Beki wao Sergio Ramos hatahama.
Mwezi Juni Manchester United ilitoa Ofa ya Pauni Milioni 28.6
kumnunua Beki huyo wa Kimataifa wa Spain na Ofa hiyo kugomewa na Real.
Hivi sasa Man United wanaisuka upya Timu yao chini ya Meneja Louis
van Gaal na tayari wameshanunua Wachezaji wapya Wanne, ambao ni Viungo
Bastian Schweinsteiger na Morgan Schneiderlin, Fulbeki wa Kulia Matteo
Darmian na Winga Memphis Depay, huku Robin van Persie na Nani wakiiuzwa
kwa Klabu ya Uturuki Fenerbahce.
Ilitarajiwa Sergio Ramos atatua Man United huku Kipa wao David De
Gea akienda Real lakini inaelekea Dili hii imekwama huku kila upande
uking'ang'ania matakwa yake.
Lakini Wachambuzi wengi walikuwa na imani kuwa nia halisi ya Ramos
si kuhama Real bali kuishinikiza Klabu hiyo iboreshe Mkataba wake.
Nao Man United hawana nia yeyote ya kumuuza David De Gea na wako
tayari kukaa nae hadi mwishoni mwa Msimu ujao ambapo Mkataba wake
utakapoisha na aondoke bure tu.
Hata hivyo zipo pia habari kuwa ikiwa De Gea ataondoka hivi sasa
basi Man United inataka ilipwe si chini ya Pauni Milioni 33 ili kumfanya
Kipa huyo awe wa Bei ghali katika Historia na kupiku Dau ambalo
Juventus lilitoa kumnunua Kipa wao Gianluigi Buffon kutoka Parma Mwaka
2001 walipolipa Pauni Milioni 32.1
Akiongea kuhusu Ramos, ambae Real wamesafiri nae kwenye Ziara yao
huko Australia, Benitez amesema: "Mengi yamezungumzwa kuhusu Ramos.
Kwangu mimi Rais ashatamka anabakia Real. Namuona Ramos kama sehemu
muhimu ya mipango yetu hapa Real. Yeye ni mshindi na hilo ndio tunataka
kwa Timu yetu. "
0 comments:
Post a Comment