Mwigizaji
wa filamu za vichekesho wa Kenya Benson Wanjau maarufu kama Mzee Ojwang
(pichani) amefariki dunia Jumapili jioni katika hospitali ya Taifa ya
Kenyatta National alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Taarifa kutoka NAirobi zinasema alikuwa anaumwa "Nimonia" (Pneumonia).
Marehemu
Mzee Ojwang alijipatia umaarufu mkubwa Afrika Mashariki kwa vituko
vyake kwenye filamu za Vitimbi, Vioja Mahakami, Vituko na Kinyonga.
Alikuwa
haonekani kwa muda mrefu kwenye televisheni za Kenya na mashabiki wake
wakiwemo wa Tanzania walikuwa hawaishi kumuulizia aliko bila kupata
jibu.
Mola aiweke Mahali pema roho
ya Mzee Ojwang - Amin.
0 comments:
Post a Comment