MTENDAJI
MKUU wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge, ametangaza kuwa
wamekubaliana na Manchester United kuhusu kumuuza Nahodha wa Germany,
Bastian Schweinsteiger taarifa ambazo pia zimethibitishwa huko Old
Trafford kupitia Tamko rasmi kwenye Tovuti yao.
Schweinsteiger, mwenye Miaka 30, alikuwa pamoja na Meneja wa Man
United Louis van Gaal huko Bayern kati ya Miaka 2009 na 2011 wakati Van
Gaal alipokuwa Meneja na wana uhusiano mzuri sana.
Kauli hii ya Rummenigge inadhihirisha makubaliano ya pande hizo
mbili kuhusu Ada ya Uhamisho ambayo inasemekana ni Pauni Milioni 6.
Mapema hii Leo, Gazeti kubwa huko Germany, Bild, liliripoti kuwa
Schweinsteiger atasaini Mkataba wa Miaka Mitatu na Man United
utakaomlipa Pauni 140,000 kwa Wiki, ikiwa ni ongezeko kubwa kupita
Bayern, na alikuwa akisubiri kuruka kwenda Jijini Manchester kupimwa
Afya pindi tu Klabu hizo zikiafikiana Ada yake ya Uhamisho.
Gwiji huyo wa Germany alikuwa amebakiza Mwaka mmoja tu kwenye Mkataba wake na Bayern.
Kufuatia uthibitisho huu, Schweinsteiger, akifuzu upimwaji Afya na
taratibu nyingine, atakuwa Mchezaji wa 3 kutua Man United baada ya
Memphis Depay na Matteo Darmian ambae nae pia yuko hatua za mwisho
kukamilisha Uhamisho wake kutoka Torino ya Italy.
0 comments:
Post a Comment