Barcelona imemsaini Nahodha wa Turkey, Arda Turan, kwa Mkataba wa
Miaka Mitano kutoka Atlético Madrid kwa Dau la awali la Pauni Milioni
24.1.
Kiungo huyo mwenye Miaka 28 amekuwa akiandamwa na Klabu kubwa huko
Ulaya, ikiwemo Chelsea, baada ya kutobolewa anataka kuihama Atletico.
Dili ya kumnunua Turan imegubikwa na utata kwani hivi sasa
Barcelona ipo kwenye Uchaguzi wa Rais wake na hivyo inaendeshwa na
Kamisheni maalum hadi atakapopatikana Rais mpya na ilibidi Kamisheni
hiyo ndio ipitishe uamuzi wa kumsaini Turan.
Lakini pia Dili hii ina Kipengele cha ajabu kwenye Mkataba wa Turan
ambacho kinatamka yeyote atakaeshinda Urais wa Barcelona kwenye
Uchaguzi hapo Julai 18 anaweza, ndani ya Siku 2 tokea hapo, kumuuza tena
Turan kwa Atletico kwa Dau la pungufu ya Asilimia 10 ya Ada ya Uhamisho
iliyolipwa.
Hata hivyo, kutokana na Adhabu ya FIFA ya kuifungia Barcelona
kutonunua Wachezaji hadi Mwakani, Turan hawezi kuichezea Barcelona hadi
Januari 2016.
0 comments:
Post a Comment