Na Mwandishi Wetu, Mwananchi
Zanzibar. Baraza
la Mitihani nchini Necta leo limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato
cha sita na kusema kuwa umefaulu umeongezeka kwa asilimia 0.61.
Akitangaza
matokeo hayo mjini Zanzibar leo, Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles
Msonde alisema mwaka huu idadi ya ufaulu ni asilimia 98.87
ikilinganishwa na asilimia 98.26.
Dk
Msonde alisema jumla ya watahiniwa 38,853 wamefaulu mitihani hiyo kati
ya watahiniwa 40,753 waliofanya mitihani hiyo ya kumaliza kidato cha
sita. Aliongeza kuwa kuna watahiniwa 35 ambao walishindwa kufanya
mitihani yao baada ya kuugua ghafla. Dk Msonde aliongeza kuwa kati ya
waliofaulu, wasichana ni 11,734 na wavulana ni 27,119.
0 comments:
Post a Comment