Maofisa wa polisi wakiwa eneo la tukio lilipotokea shambulio lililoua watu 14 usiku wa kuamkia leo.
Takribani
watu 14 wameuawa, 11 wakijeruhiwa baada ya Al-Shabaab kushambulia
kijiji cha Soko Mbuzi kilichopo jirani na Mji wa Mandera nchini Kenya
usiku wa kuamkia leo. Mamlaka husika huko Mandera yathibitisha.
Mashuhuda
wa tukio hilo wameeleza kuwa shambulio lilitokea saa 7 usiku wa kuamkia
leo wakati wakazi wa Kijiji cha Soko Mbuzi wakiwa wamelala.
Shambulio hilo limeelezwa kuwalenga wafanyakazi wa machimboni ambao wengi wao siyo wenyeji.
Taswira kutoka Kijiji cha Soko Mbuzi lilipotokea shambulio.
Wananchi wakiwa eneo hilo la tukio.
(Picha zote na Daily Nation)
0 comments:
Post a Comment