Manchester United wako njiani kumpa mkono Straika wao
Robin van Persie ambae tayari kuna makubaliano ahamie Uturuki Klabuni
Fenerbahce.
RVP
Tayari Fenerbahce ishakubaliana Mkataba wa Miaka Minne na Robin van Persie ili ahamie hapo kutoka Manchester United.
Hivi karibuni, Mkurugenzi wa Fenerbahce, Guiliano Terraneo, alitua
huko England kukamilisha Dili hiyo na Van Persie, Raia wa Netherlands
mwenye Miaka 31, ambae Mkataba wake wa sasa na Man United umebakiza
Mwaka mmoja tu.
Ikiwa Dili hii itakamilika, basi Van Persie ataungana huko Uturuki
na Mchezaji mwingine aliekuwa Man United, Nani, ambae Siku mbili
zilizopita alihamia Fenerbahce kwa Dau la Pauni Milioni 4.5.
Lakini kuhama kwa Robin van Persie kutaifanya Man United ibaki na
Mafowadi wanaotambulika Wawili tu, Kepteni Wayne Rooney na Chipukizi
James Wilson.
Fowadi wao mwingine aliebaki ni Javier Hernandez 'Chicharito' ambae
Msimu uliopita alitupwa kwa Mkopo huko Real Madrid na sasa anapaswa
kurudi Old Trafford lakini Wiki iliyopita alivunjika Mfupa wa Begani na
kufanyiwa Operesheni itakayomweka nje kwa takriban Miezi Miwili.
0 comments:
Post a Comment