Meneja
wa Manchester United Louis van Gaal Leo, kwa mara ya kwanza tangu Timu
ikusanyike kwa ajili ya Mazoezi kwa Msimu mpya, ataongea na Wanahabari
huko Jijini Manchester.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, Van Gaal pia atamtambulisha rasmi
Mchezaji mpya wao, Memphis Depay, waliemnunua Mwezi uliopita kutoka PSV
Eindhoven ya Holland.
Huku kukiwa na habari tele za Man United kumnasa Beki wa Kimataifa
wa Italy, Matteo Darmian, anaechezea Torino, ambae Leo anasemekana
atapimwa Afya yake, na pia kuuzwa kwa Robin van Persie kwa Fenerbahce na
Angel Di Maria kwa PSG, Wadau wa Man United wana shauku kubwa kujua Van
Gaal atatoboa kipi zaidi.
Shauku hiyo pia inakolezwa na zile habari za kila Siku za Man
United kuhusishwa na kununua Wachezaji wapya wakitajwa sana Mastaa kama
Nicolas Gaitan, Nicolas Otamendi, Morgan Scneiderlin na lukuki kadhaa
wengine.
Man United inatarajiwa kuruka kwenda Marekani Jumatatu Julai 13
kuanza Ziara yao na pia kutetea Taji lao la International Champions Cup
walilotwaa Mwaka Jana huko huko USA.
0 comments:
Post a Comment