Fabio Capello ameondolewa kama Kocha Mkuu wa Russia baada kushika wadhifa huo kwa Miaka Mitatu.
Mwaka Jana, Capello alisaini nyongeza ya Mkataba wake kwa Miaka
Minne ambao ungemweka huko Urusi hadi baada ya Fainali za Kombe la Dunia
za Mwaka 2018 ambazo Urusi ndio Wenyaji wake.
Lakini, baada ya matokeo mabovu, ambayo yameifanya Russia iwe na
Pointi 8 tu katika Mechi 6 za kufuzu Fainali za EURO 2016, Russia
imestuka.
Hata huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia Mwaka Jana
Russia, chini ya Capello, ilitupwa nje hatua za Makundi tu bila ya
kushinda hata Mechi moja katika Mechi zao 3.
Chama cha Soka cha Russia (RFU kimesema kimefikia makubaliano na
Kocha huyo kutoka Italy, ambae pia aliwahi kuifundisha England,
kuutengua Mkataba wake.
Inaaminika RFU imemlipa Capello Euro Milioni 15 kufuatia uamuzi huo.
Mwezi uliopita, Mashabiki wa Russia walianzisha kampeni ya kuchangishana Fedha ili kuununua Mkataba wa Capello na kumng'oa.
0 comments:
Post a Comment