Real
Madrid imetangaza kuwa Kipa wao Iker Casillas aliewadakia Mechi 725
anahamia FC Porto ya Ureno baada ya Klabu hizo mbili kukubaliana.
Casillas, mwenye Miaka 34 na ambae ni Nahodha wa Real na Timu ya
Taifa ya Spain, alijiunga na Timu ya Vijana ya Real Mwaka 1990 na
kubakia hapo hapo akitwaa Mataji makubwa 17.
Real, licha ya kutangaza kuondoka kwa Kipa huyo mkongwe, pia ilitoa taarifa ndefu ya kumsifia Kipa huyo na kumuaga rasmi.
Mwanzo wa mwisho wa Casillas hapo Real ulianzia kwenye himaya ya
Jose Mourinho ambae alimtema na kumpiga Benchi lakini baada ya Mourinho
kuondoka Kipa huyo akarudia tena kuwa KIpa Nambari Wani.
Hivi sasa Real ipo mbioni kuwawinda Makipa wawili, Kiko Casilla wa Espanyol na David De Gea wa Manchester United.
0 comments:
Post a Comment