Liverpool
imeamua kutomchukua Winga wao Raheem Sterling kwenye Ziara yao ya huko
Mashariki ya Mbali na Australia ambayo Leo hii wanapaswa kusafiri wakati
Manchester City ikipandisha Dau lao la kumnunua na kufikia Pauni
Milioni 45.
Awali Man City ilitoa Ofa mbili, zote zikikataliwa, na ya mwisho
ilikuwa ni Pauni Milioni 40 wakati Liverpool wanamthamini Mchezaji huyo
kuwa ni Pauni Milioni 50.
Ripoti toka huko England zinadaia Mchezaji huyo ameachwa kwenye
Ziara ili akamilishe Uhamisho huu kwenda City baada ya Majuzi
kutoonekana Mazoezini kwa Siku 2 akidai Mgonjwa na Ijumaa kuibuka tena
Mazoezini.
Sakata la Sterling na Liverpool lilianzia Januari alipogomea
Mkataba mpya ambao ungemlipa Mshahara kwa Wiki wa Pauni 100,000 toka
35,000 za sasa.
Baada ya hapo, Wakala wa Sterling, Aidy Ward, akachochea zaidi kwa
kudai Sterling hatasaini Mkataba wowote mpya hata akilipwa Pauni Laki 9
kwa Wiki kitu ambacho Liverpool kiliwaudhi sana na kumsusia Wakala huyo.
0 comments:
Post a Comment