Meneja
mpya wa West Ham Slaven Bilic Leo atakuwa Benchi kwa mara ya kwanza
wakati Timu yake ikicheza Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Kwanza ya
Mtoano ya EUROPA LIGI huko Nchini Andorra dhidi ya Lusitanos.
Katika Mechi ya kwanza iliyochezwa Upton Park Jijini London Wiki
iliyopita, West Ham iliinyuka Lusitanos 3-0 huku Slaven Bilic akikaa
Jukwaani na kumpisha Terry Westley, Kocha wa Vijana, kuongoza Timu.
Kitendo hicho cha Bilic kukaa Jukwaa la Watazamaji katika Mechi
hiyo ya kwanza kilimkera mno Kocha wa Lusitanos, Xavi Roura, ambae
alidai ni kuwavunjia heshima.
Kama ilivyo katika Mechi ya kwanza, hii Leo West Ham, ambao tayari
wametangaza Wachezaji 11 watakaocheza, kitakuwa mchanganyiko wa Vijana
na Maveterani wa Timu ya Kwanza wakiwemo Joey O'Brien, ambae hii itakuwa
Mechi yake ya 100 kwa West Ham, na wengine ni James Tomkins, Morgan
Amalfitano na Diafra Sakho, aliefunga Bao 2 katika Mechi ya kwanza.
Mmoja wa Vijana watakaocheza ni Lewis Page, mwenye Miaka 19, wakati Beki wa Miaka 16, Reece Oxford, akiwekwa Benchi.
Mbali ya Mechi hii ya West Ham na Lusitanos, pia Leo zipo Mechi
nyingine za 50 za Marudiano za Raundi ya Kwanza ya Mtoano ya EUROPA
LIGI.
KIKOSI CHA WEST HAM KITAKACHOANZA LEO: Randolph, O'Brien, Tomkins,
Burke, Page, Amalfitano, Poyet, Cullen, Jarvis, Lee, Sakho. Subs:
Spiegel, S Westley, Knoyle, Oxford, Nasha, Parfitt-Williams, Brown.
0 comments:
Post a Comment