Nani mbunge
halali wa Vunjo? kumbuka baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 James Mbatia
alitangazwa mshindi wa jimbo la Vunjo ambalo lilikua chini ya Mrema
kipindi kilichopita, baada ya huo ushindi Mrema alifungua kesi
Mahakamani baada ya kudai amechezewa mchezo mchafu na yeye ndio
alistahili kuwa mshindi.
Kesi ikaendelea mpaka leo April 4 2016 maamuzi mapya kutangazwa kwamba Mahakama kuu kanda ya Moshi imeridhia makubaliano yaliyofikiwa kati ya Mbunge wa Vunjo James Mbatia na Agustino Mrema hivyo Mahakama chini ya jaji Lugano Mwandambo imeridhia shauri hilo kuisha na kwamba James Mbatia ndiye Mbunge halali wa Vunjo na Mrema atatakiwa kulipa sehemu ya gharama za mawakili wa Mbatia shilingi Milioni 40.
Mrema hakuonekana Mahakamani leo na aliwakilishwa na Wakili wake January Nkobogo ambapo James Mbatia aliyehudhuria Mahakamani leo alisema yafuatayo >>> ‘siku
ya leo tumeandika historia mpya hasa kwa jimbo letu la Vunjo, kwa kuwa
ukweli ni msingi wa haki na Wanasheria wetu sita waliokua wananitetea
mimi‘
‘Baada ya mlalamikaji
Mzee wetu Mrema kufikia hatua ya kutoa ushahidi Mahakamani baada ya
ushahidi alioutoa Mahakamani na maswali aliyoulizwa yeye mtu mzima
akaona upepo sio mzuri kwa upande wake, alipoliona hilo kiutu uzima
baada ya kushauriwa na kuona jasho lililomtoka Mahakamani wiki iliyopita
akaona hali inazidi kuwa mbaya upande wake‘
James Mbatia kwenye sentensi nyingine amesema >>> ‘Ndugu
Mrema amekubali au kukanusha yale yote aliyoleta Mahakamani na ushahidi
wake wote aliosema Mahakamani na malalamiko dhidi yangu, Wanavunjo,
dhidi ya taasisi za kidini yooote ameyakanusha kwenye hati ya
makubaliano, hilo ndio lilikua la msingi ameyakanusha na amesaini
mwenyewe’
‘La
pili, Mrema amekubali kuwa James Mbatia ndio mbunge halali
aliyechaguliwa jimbo la Vunjo, swala la tatu alilokubali ni kweli
tungeweza kumdai gharama kubwa, mimi binafsi nimeingia gharama kubwa
ikiwemo ya usafiri toka November 2015 alivyoleta shauri hili Mahakamani,
sijamdai gharama kwa upande wangu hata senti moja, nimemsamehe kama
kawaida yangu‘ – James Mbatia
Cha kumalizia Mbatia amesema ‘Kuna
gharama kubwa ambazo ziliingia upande wa jopo lote la Mawakili na
amekubali yeye mimi nilipe asilimia 50 ya gharama za mawakili na yeye
alipe 50, kwahiyo Mrema amekubali kulipa Mawakili sehemu tu ya gharama
ya MILIONI 40 kwa Mawakili wetu na ni agizo la Mahakama na imeingia
Mahakamani, kwa hatua ya kwanza MILIONI 15 Mawakili wetu watazipata kwa
sababu zipo Mahakamani tayari aliziweka deposit, May atalipa nyingine 15
na kabla ya June atalipa 10 zilizobaki na asipofanya hivyo ni kifungo’
0 comments:
Post a Comment