Home » » EWURA Yashusha bei za Umeme .....Service Charge Yafutwa

EWURA Yashusha bei za Umeme .....Service Charge Yafutwa

 

Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imetangaza kushusha bei za umeme kuanzia leo kwa watumiaji wote wa viwango tofauti.
Kushuka huko kwa bei ya umeme ni kutokana na ombi la Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kutaka bei za umeme zipunguzwe sambamba na hilo gharama za huduma kwa baadhi ya wateja zimeondolewa. 
Bei mpya  kwa watumiaji wadogo ni sh.100 kwa uniti, watumiaji wa kati ni sh.292  toka  298  ya  zamani.Wafanyabiashara wadogo ni sh. 195 toka sh. 200  ya  hapo  awali.
Bei mpya  kwa wafanyabiashara wa kati ni sh.157 toka sh. 159. Wanaonunua kwa wingi (bulk) ni sh. 152  toka  sh. 156  ya  hapo awali
Tazama jedwali  hili  kuona mgawanyo  wa  bei  mpya.
Toa maoni yako kwa habari hii kwa kuweka email yako hapa,na endelea kutufatilia zaidi Ukurasa wa habari

0 comments:

 
Supported by AMAGA Media services : | |
Copyright © 2015. UKURASA WA HABARI - All Rights Reserved
Templete Designed by Abdallah Magana
Proudly powered by Blogger