Michezo ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imeendelea tena usiku wa April 6 2016 kwa michezo miwili kupigwa, klabu ya Real Madrid ya Hispania ililazimika kusafiri kutoka Hispania hadi Ujerumani kucheza dhidi ya wenyeji wao Wolfsburg.
Real Madrid ambao weekend iliyopita walikuwa na furaha ya kuifunga FC Barcelona 2-1 katika uwanja wa Nou Camp, wamekubali kipigo cha goli 2-0 kutoka kwa Wolfsburg, Real Madrid walianza kufungwa dakika ya 18 na Ricardo Rodriguez kwa mkwaju wa penati na baadae Maximilian Arnold kuwafunga dakika ya 25.
Kwa sasa Real Madrid watakuwa na mtihani wa kuifunga Wolfsburg kwa goli zaidi ya mbili katika mchezo wa marudiano utakaochezwa Santiago Bernabeu April 12 2016 ili waweze kufikia hatua ya nusu fainali ya michuano ya klabu Bingwa Ulaya,
Cristiano Ronaldo alizibitiwa na mabeki wa Wolfsburg, Kama utakuwa unakumbuka vizuri Ronaldo baada ya kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya FC Barcelona katika mchezo wa El Clasico weekend iliyopita alinaswa katika vyumba vya kubadilishia nguo akishangilia akiwa kavaa nguo ya ndani pekee.
Video ya magoli ya Wolfsburg Vs Real Madrid
0 comments:
Post a Comment