SIKU MBEYA CITY ILIPOINGIA MKATABA NA BIN SLUM, HAPA ILIWAKILISHWA NA MMOJA WA WAKURUGENZI WAKE, MOHAMMED BIN SLUM (KULIA). |
Mdhamini
wa Mbeya City, Nassor Bin Slum amesema anatarajia kuongeza mkataba
mwingine wa miaka miwili ya kuidhamini timu hiyo iwapo itabakia ligi kuu
msimu ujao.
Mbeya
City, ambayo ilikuja kwa kasi wakati ilipopanda ligi kuu msimu wa
2013/14 na kumaliza ikiwa nafasi ya tatu ya msimamo wa iliingia udhamini
na Bin Slum kwa muda wa miaka miwili ambao unatarajia kufikia tamati
mwishoni mwa msimu huu.
NASSOR BIN SLUM |
Hata
hivyo, timu hiyo ipo nafasi ya 12 ya msimamo kwa sasa ikiwa na pointi
24 nyuma ya Kagera Sugar yenye pointi 25 na iwapo itafanya vibaya katika
mechi zake zilizobakia itakuwa kwenye hatari ya kushuka daraja.
Bin
Slum amesema kuwa, timu hiyo haifanyi vizuri lakini ameridhika na jinsi
inavyomtangaza ikiwa ni pamoja na kuheshimu mkataba walioingia na kudai
kuwa ataongeza mkataba mwingine wa miaka miwili iwapo timu hiyo itabaki
ligi kuu msimu ujao na ikishuka ndiyo anaagana nayo.
“Timu
haifanyi vizuri, lakini naridhika na kwa jinsi wanavyonitangaza vyema
katika kila mechi wanayocheza, ni watu wanaoheshimu mkataba, Mbeya City
wanajitahidi, nitaongeza mkataba mwingine nikimaliza huu na nimewapa
masharti, wamesema watajipanga ili kurudisha makali yao ya msimu
uliopita.
“Kasi
waliyoionyesha msimu huu ni tofauti na msimu uliopita, lakini kwa sasa
nipo katika mazungumzo ya kuongeza mkataba mwingine wa miaka miwili
ijayo.
“Mkataba
wa safari hii nitakaoingia nao utakuwa ni wa masharti tofauti na
ilivyokuwa hapo nyuma na iwapo watashuka daraja basi itakuwa ndio mwisho
umefikia kwani moja ya masharti yangu ni kudhamini timu ambazo zipo
ligi kuu tu,” alisema Bin Slum.
Credit:Salehe jembe
0 comments:
Post a Comment