Ndanda
FC imeonyesha si laini baada ya kuilazimisha sare ya mabao 2-2 Azam FC
katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi
jijini Dar es Salaam.
Azam
FC ilitangulia kufunga mabao mawili kupitia Ramadhani Singano ‘Messi’
na Didier Kavumbagu na kuonyesha dalili ingeweza kushinda hata mabao
manne.
Lakini
juhudi hizo zikakwama baada ya Atupele Green kusawazisha kwa bao la
penalti kabla ya Hemed Msumi aliyeingia kipindi cha pili kufunga bao la
pili.
“kuchacha”
kwa kiporo hicho kuinaifanya Azam FC kufikisha pointi 54 baada ya mechi
23, hivyo inalazimika kushinda mechi yake ya 24 ili kuifikia Simba
iliyo kileleni ikiwa na pointi 57.
Sare hiyo imeifanya Yanga isogee katika nafasi ya pili juu ya Yanga yenye pointi 53, lakini ina mechi moja nyuma kwa Azam.
Sare hiyo imeifanya Yanga isogee katika nafasi ya pili juu ya Yanga yenye pointi 53, lakini ina mechi moja nyuma kwa Azam.
0 comments:
Post a Comment